Ukraine: Zelensky na Lula washindwa kukutana kwa mazungumzo Hiroshima
Mkutano kati ya Rais wa Ukraine Zelensky na mwenzake wa Brazil Lula haukufanyika huko Hiroshima, nchini Japan. Rais wa Brazil Lula da Silva anasema alimsubiri mwenzake wa Ukraine kando ya mkutano wa nchi zilizostawi zaidi kiviwanda, G7, lakini hakuja.
Imechapishwa:
Na mwandishi wetu huko São Paulo, Martin Bernard
Rais wa Ukraine alichukua fursa ya safari yake ya Japan kukutana na viongozi wengi, akiwemo Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, ambaye alikataa kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Msimamo wa Brazil ni tofauti: Lula anatambua kuwa Moscow ni mchokozi, lakini anataka kumaliza vita kwa njia ya mazungumzo, na sio kwa kuzidisha mzozo - wakati G7 ndiyo kwanza imejitokeza kuunga mkono mauzo mapya ya silaha kwa Ukraine.
Tukio hili la wawili hao kushindwa kukutana hukoHiroshima linakuja wiki moja baada ya mshauri wa kidiplomasia wa Lula kusafiri kwenda Kyiv. Celso Amorim kisha akaelezea msimamo wa Brazil… Baada ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi huko Brasilia, Sergei Lavrov, mwezi uliopita.
Baada ya mkutano wa G7, mpango wa Lula kuunda "klabu ya amani" kwa Ukraine bado unaonekana kukwama.