Pata taarifa kuu

Ulaya: Viongozi wa Taiwan na Paraguay waahidi kuimarisha Diplomasia

Nairobi – Kiongozi wa Taiwan, Tsai Ing –Wen ampongeza Rais mpya wa Paraguay, Santiago Pena kwa njia ya simu na kuhakikisha mahusiano mazuri kati ya kisiwa hicho na mshirika wake peke wa kidiplosmaisa huko kusini mwa Marekani .

Santiago Pena wa chama tawala cha Colorado ateuliwa kuwa rais mpya wa Paraguay .
Santiago Pena wa chama tawala cha Colorado ateuliwa kuwa rais mpya wa Paraguay . REUTERS - AGUSTIN MARCARIAN
Matangazo ya kibiashara

Mchumi na waziri wa zamani wa fedha Pena ameapa kuendelea kuitambua Taiwan, na ushindi wake ulifuta hofu ya Taipei kwamba Paraguay ingeachana na kisiwa hicho kinachojitawala na kupendelea Beijing.

Mpinzani wake Efrain Alegre alikuwa amependekeza mabadiliko ya utii kwa Uchina, ambayo inadai kuwa  Taiwan ni  sehemu ya eneo lake na kushinikiza kuitenga kimataifa.

Wakati wa mazungumzo yao ya dakika 20, Tsai alimpongeza Pena na kumshukuru kwa "kuonyesha msimamo wake thabiti wa kudumisha na kuimarisha uhusiano wa Taiwan na Paraguay", ofisi yake ilisema.

Pena alimwambia Tsai kuwa anatazamia kuzuru Taiwan na kukutana naye "haraka iwezekanavyo", na anatumai  wataimarisha ushirikiano,".

"Ninatarajia kufanya kazi nanyi ili kuendeleza ushirikiano wetu wa nchi mbili na ustawi wa watu wetu," Tsai aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter baada ya mazungumzo yao ya  simu .

Paraguay ni mojawapo ya washirika wachache wa Taiwan waliosalia katika kusini mwa Marekani baada ya Panama, El Salvador, Jamhuri ya Dominika, Nicaragua na Honduras kubadili utii kwa China katika miaka ya hivi karibuni.

Kusini mwa Marekani  imekuwa uwanja muhimu wa vita vya kidiplomasia kwa China na Taiwan tangu kumalizika kwa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Uchina mnamo 1949.

Beijing imetumia miongo kadhaa kuwashawishi washirika wa kidiplomasia wa Taipei kubadili upande, tangu Tsai aingie madarakani mwaka 2016.

Honduras ilihamia Beijing mwezi Machi, na kuacha nchi 13 pekee zinazoitambua Taipei kidiplomasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.