Pata taarifa kuu

Urusi: Moto mkubwa umeripotiwa katika ghala la mafuta la Crimea : Mamlaka

NAIROBI – Moto mkubwa umezuka katika mji wa bandari wa Crimea katika eneo la Sevastopol kufuatia shambulio linalodaiwa kuwa huenda limetekelezwa na ndege isiyo na rubani kwenye tanki la kuhifadhia mafuta, Mikhail Razvozhayev, gavana anayegemea upande wa nchi ya Urusi ameandika kupitia Telegram.

Mamlaka katika mji wa Crimea zinasema moto mkubwa katika ghala la mafuta umesababishwa na ndege zisizokuwa na rubani
Mamlaka katika mji wa Crimea zinasema moto mkubwa katika ghala la mafuta umesababishwa na ndege zisizokuwa na rubani AP
Matangazo ya kibiashara

"Ghala la mafuta linawaka ... Kulingana na ripoti za awali, shambulio la ndege isiyo na rubani huenda limesababisha moto huo," ameandika kiongozi huyo.

Ukraine imetangaza mara kwa mara nia yake ya kutwaa tena eneo la Crimea, ambalo Urusi ililitwaa kinyume cha sheria mwaka.

Sevastopol ni eneo kunakopatikana Bahari nyeusi ya Urusi na limekumbwa na mfululizo wa mashambulio ya ndege zisizo na rubani tangu mashambulio ya Kremlin nchini  Ukraine kuanzishwa mwaka jana.

Mapema wiki hii, Urusi ilisema "imezuia" shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye bandari hiyo. Urusi ilitwaa Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014.

Urusi imeendelea kutekeleza mashambulio ya makombora nchini Ukraine ikizionya nchi za Magharibi kuacha kuisaidia Ukraine ikisema kuwa hatua hiyo inaweza kuchochea mzozo zaidi.

Ukraine kwa upande wake imekuwa ikizitaka nchi washirika wake kuihami ilikupiga jeki juhudi zake za kujilinda kutokana na mashambulio ya Urusi.

Mataifa ya Magahribi yamekuwa yakitoa ahadi ya kuisaidia Kyiv na silaha za kujeshi na fedha kuimarisha ngome zake za ulinzi.

Wito umekuwa ukitolewa kwa rais wa China Xi Jiping ambaye ni mshirika kwa karibu wa rais wa Urusi Vladmir Putin, kumshawishi kiongozi huyo kusitisha mapigano nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.