Pata taarifa kuu

Washington yaomba 'kuachiliwa mara moja' kwa mwandishi wa habari wa WSJ anayezuiliwa nchini Urusi

Marekani inaendelea kudai "kuachiliwa mara moja" kwa mwandishi wa habari wa Marekani wa Gazeti la "Wall Street Journal" Evan Gershkovich ambaye kuzuiliwa kwake nchini Urusi 'kinyume cha sheria', ametangaza, Jumanne Aprili 18, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony kando ya matokeo wa G7 nchini Japan, shirika la habari la AFP limeripoti.

Mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich, Julai 24, 2021 akiwa katika eneo lisilojulikana.
Mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich, Julai 24, 2021 akiwa katika eneo lisilojulikana. © Dimitar DILKOFF / AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya kwanza, balozi wa Marekani huko Moscow, Lynne Tracy, aliweza kumtembelea Jumatatu Bw. Gershkovich, ambaye anazuiliwa kwa zaidi ya wiki mbili na kushtakiwa kwa ujasusi na mamlaka ya Urusi. Kesi yake dhidi ya kuzuiliwa kwake imepangwa kusikilizwa katika ngazi ya rufaa leo Jumanne.

"Yuko katika afya njema na ana anaendelea vizuri licha ya mazingira aliyomo," Bi Tracy ameandika kenye ukurasa wake wa Twitter baada ya kukutana na mfungwa huyo mwenye umri wa miaka 31. Evan Gershkovich, mwandishi wa Gazeti la Wall Street Journal huko Moscow na ambaye hapo awali aliwahi kufanya kazi na shirika la habari la AFP, alikamatwa na vyombo vya usalama vya Urusi mnamo Machi 30 akiwa kazini huko Yekaterinburg katika eneo la  Urals.

Mamlaka ya Urusi ilimshutumu hasa kwa kukusanya habari juu ya tasnia ya ulinzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.