Pata taarifa kuu

Mageuzi ya pensheni: Siku ya 12 ya mgomo katika mkesha wa uamuzi wa Baraza la Katiba

Miezi mitatu baada ya kutangazwa kwa mageuzi ya pensheni nchini Ufaransa, Baraza la Katiba linatarajia kuchukua uamuzi siku ya Ijumaa Aprili 14 juu ya uhalali wa Nakala iliyopitishwa hivi karibuni na Bunge. Wakati huo huo, muungano wa vyama unatoa wito Alhamisi hii kwa siku ya kumi na mbili ya uhamasishaji wa kitaifa.

Watu wakiandamana dhidi ya mageuzi ya pensheni huko Paris, Februari 11, 2023.
Watu wakiandamana dhidi ya mageuzi ya pensheni huko Paris, Februari 11, 2023. Β© AP/Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

Muda wa kupata ukweli umewadia kwa vyama vya wafanyakazi. Miezi mitatu baada ya kuanza kwa uhamasishaji wa "kihistoria" dhidi ya mageuzi ya pensheni, Baraza la Katiba litachukua uamuzi siku ya Ijumaa jioni kuhusu uhalali wa muswada wa sheria uliyopitishwa Bungeni baada ya kutumia Ibara ya 49-3. Wakati huo huo, muungano wa vyama vya wafanyakazi unaandaa siku mpya ya uhamasishaji Alhamisi hii, siku ya kumi na mbili tangu mwishoni mwa mwezi Januari. Labda itakuwa hatua ya mwisho kabla ya mpango huo wa serikali kuanza kutekelezwa. Katibu mkuu wa CFDT, Laurent Berger, kwa vyovyote vile hajapuuza uwezekano huu. "Mtasubiri hadi mwanzoni mwa wiki ijayo ili kupata jibu la swali hili," alijibu kwenye kituo cha LCI siku ya Jumanne.

Mamlaka inatarajia kuona kati ya waandamanaji 400,000 na 600,000 kote nchini. Wiki iliyopita, walikuwa 570,000 walioingia mitaani kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani, milioni 2 kulingana na muungano wa vyama vya wafanyakazi wa CGT. Huko Paris, maandamano yataanzia Place de l'OpΓ©ra na kujiunga na waandamanaji wengine kutoka Bastille. Kudororora kwa shughuli kunatarajiwa katika shirika la reli la SNCF, kwa wastani treni za mwendo kasi nne kati ya tano, na aina nyingine ya treni ya TER tatu kati ya tano. Safari za ndege pia zinatarajia kufutwa katika viwanja vya ndege vya Nantes, Bordeaux na Toulouse. Muungano wa vyama vya wafanyakazi CGT pia unatoa wito wa mgomo wa saa 24 katika mitambo yote ya kusafisha.

Sio suala la kuweka shinikizo kwa majaji wa Baraza la Katiba, amesema Cyril Chabanier, mkuu wa muungao wa CFTC, lakini kuwatumia ujumbe: kuonyesha kwamba hali ya wasiwasi inaripotiwa katika jamii na uamuzi wa raia mambo mengine, na tunahimiza tu ili kuondoa dosari katika nakala hii. β€œTunaonyesha hasira hizi siku moja kabla, lakini hatutii shinikizo, kwa sababu hatuhoji uhalali wa taasisi hiyo ambayo ni muhimu zaidi katika nchi yetu,” ameongeza.

Chaguzi tatu

Matukio matatu yapo kwenye mezani: kuidhinishwa kwa muswada huu wa sheria, kuondoa kwa sehemu au kuondoa kwa kamili. Baraza la Katiba linatarajiwa pia kutoa uamuzi ikiwa ombi la mrengo wa kushoto la kura ya maoni ya mpango wa pamoja (RIP) linakubalika au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.