Pata taarifa kuu

Mageuzi ya pensheni: Seneti yapiga kura kuongeza umri wa kustaafu hadi 64

Bunge la Seneti nchini Ufaransa, lenye idadi kubwa ya maseneti kutoka mrengo wa kulia, limepitisha hivi punde Jumatano, Machi 8 usiku, baada ya vita vikali vya kiutaratibu na upande wa kushoto, kifungu muhimu cha mradi wa mageuzi ya pensheni, na kuongeza kutoka miaka 62 hadi 64 umri wa kisheria wa kustaafu.

Kikao cha Bunge la Seneti nchini Ufaransa wakati wa majadiliano juu ya mradi wa marekebisho ya pensheni, Machi 6, 2023.
Kikao cha Bunge la Seneti nchini Ufaransa wakati wa majadiliano juu ya mradi wa marekebisho ya pensheni, Machi 6, 2023. AFP - ALAIN JOCARD
Matangazo ya kibiashara

Maseneta wamepiga kura kuongeza umri wa kustaafu kutoka umri wa miaka 62 hadi 64. Kura hiyo imepitishwa kwa kura 201 dhidi ya 115 katika makao makuu ya Bunge la Seneti huko Luxembourg, Jumatano, Machi 8. Waziri Mkuu Élisabeth Borne "amekaribisha" kura hii kwenye Twitter, akisifu tena "mageuzi ya usawa na ya haki".

Bunge la Seneti limepitisha kifungu cha 7 cha mradi wa pensheni. Nimefurahiya kwamba mijadala imewezesha kufikia kura hii.

Uhakiki wa nakala hii utaendelea. Itawezesha kuchunguza mapendekezo kutoka makundi mbalimbali kwa mageuzi ya usawa na ya haki.

Upinzani unashutumu "udhibiti", upande wa kulia unakashifu "ukiukwaji wa sheria"

"Jina lako litaambatanishwa milele na mageuzi ambayo yatachukua karibu miaka 40 nyuma," mwanasoshalisti Monique Lubin alimwambia Waziri wa Kazi Olivier Dussopt. Mkomunisti Eliane Assassi alikashifu mjadala "ulioguikwa na vurugu" na "lengo" la wabunge wengi "kutenga upinzani".

Kwa mujibu wa mpango wa serikali, umri wa kustaafu wa kisheria utawekwa hatua kwa hatua kutoka 62 hadi 64, kwa kiwango cha miezi 3 kwa mwaka kuanzia Septemba 1, 2023 hadi 2030. 

Mjadala utaanza tena Alhamisi Machi 9 juu ya marekebisho yenye utata ya Bruno Retailleau. Wingi wa maseneta unalenga kupitia nakala na kura ya mwisho kufikia makataa ya Jumapili Machi 12 saa sita usiku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.