Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Ufaransa: Mamia kwa maelfu waingia mitaani kupinga mageuzi ya pensheni

Mamia kwa maelfu ya watu wameandamana katika miji mbalimbali nchini Ufaransa kupinda kile waandamanaji wanachosema mageuzi ya pensheni yasiokubalika. Haya ni maandamano ya kihistoria kwa siku ya sita kufanyika katika miji mbalimbali nchini Ufaransa dhidi ya mageuzi ya pensheni ambayo yanatetewa na Emmanuel Macron, kabla ya kupitishwa na Bunge katika siku chache zijazo.

Maandamano huko Marseille, kusini mwa Ufaransa, Jumanne Machi 7, 2023.
Maandamano huko Marseille, kusini mwa Ufaransa, Jumanne Machi 7, 2023. AP - Daniel Cole
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi cha CFDT (wanamageuzi), Laurent Berger, amekaribisha "uhamasishaji wa kihistoria" Jumanne mchana, kabla ya kuanza kwa maandamano katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris. Kando yake, mwenzake wa chama cha wafanyakazi cha CGT, Philippe Martinez, amebaini kwamba "itakuwa siku yenye uzito zaidi ya uhamasishaji tangu kuanza kwa mzozo huu".

Kitendo kikubwa cha kwanza cha siku hii, usafirishaji wa mafuta umezuiliwa asubuhi wakati malori yaliyokuwa yakijaribu kutondoka katika "viwanda vyote vya kusafisha mafuta " nchini Ufaransa, chama cha wafanyakazi cha CGT-Kemia kimeliambia shirika la habari la AFP, kikibaini kwamba mitambo ya kusafishia mafuta ya TotalEnergies, Esso-ExxonMobil na Petroineos imeathirika hasa na maandamano hayo. Wakati wa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, waandamanaji walianza kufunga barabara kuu huko Rennes, magharibi mwa Ufaransa.

Siku hii ya sita ya maandamano inapaswa pia kuadhimishwa kwa uzinduzi wa migomo inayoweza kurejelewa katika sekta kadhaa, kutoka kwa sekta ya usafiri kupitia mitambo ya kusafisha mafuta, hadi skta ya nishati, biashara na taka, na kwa maandamano ambayo yanaonekana yametekelezwa kwa sehemu kubwa ya raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.