Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Ufaransa: kwa siku ya 10, maandamano dhidi ya mageuzi ya pensheni yaendelea

Nchini Ufaransa, makumi ya maelfu ya watu wameingia tena mitaani Jumanne hii, Machi 28 kwa siku ya 10 ya uhamasishaji dhidi ya mageuzi ya pensheni. Wakati huo huo vyama vya wafanyakazi vimeomba kuwepo na "upatanishi", hata hivyo serikali imefutilia mbalia omboi hilo.

Msafara wa maandamano katika eneo la Place de la Nation mjini Paris, Machi 28, 2023.
Msafara wa maandamano katika eneo la Place de la Nation mjini Paris, Machi 28, 2023. © REUTERS/Nacho Doce
Matangazo ya kibiashara

Siku tano baada ya maandamano ya hapo awali - ambayo yalikuwa ya kihistoria na ambayo yaligubikwa na makabiliano kati ya waandamanaji na polisi - waandamanaji wamepaza tena sauti siku ya Jumanne ili madai yao kupinga mageuzi ya pensheni yaweze kusikika zaidi.

Huko Paris, kulingana na muungano wa vyama vya wafanyakazi, CGT, watu 450,000 wameandamana katika mji mkuu. Siku ya Jumanne, msafara uliondoka alaasiri katika eneo Jamhuri " Place de la République" ili kufika eneo la taifa "Place de la Nation" saa moja na nusu baadaye.

Maafisa wa polisi elfu tano na mia tano wametumwa kuisimamia (na 13,000 kote Ufaransa). Saa tisa mchana, zaidi ya kaguzi 6,000 zimefanyika na watu 18 wamekamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.