Pata taarifa kuu

Putin na Xi kujadili kuhusu vita vya Ukraine

NAIROBI – Rais wa Urusi, Vladmir Putin na mgeni wake rais wa China Xi Jinping, hivi leo wanatarajiwa kuwa na mazungumzo rasmi mjini Moscow, ambapo watajadiliana namna ya kumaliza mzozo wa Ukraine.

Vladimir Putin wa Urusi na  Xi Jinping wa China jijini Moscow Jumatatu 20 Machi 2023.
Vladimir Putin wa Urusi na Xi Jinping wa China jijini Moscow Jumatatu 20 Machi 2023. AFP - SERGEI KARPUKHIN
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo yao yanafuatia mkutano usio rasmi walioufanya hapo jana, ambapo rais Putin alimueleza mgeni Wake kuwa, yuko tayari kusikiliza mapendekezo ya Beijing kuhusu kumaliza vita kati yake na Ukraine.

Ziara ya siku tatu ya rais Jinping nchini Urusi, inatafsiriwa kama ushindi kwa Putin, na imekuja siku chache kupita tangu mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita ICC, ito hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo.

Tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, utawala wa beijing umekuwa ukijaribu kujionesha kuwa hauna upande katika mzozo unaoendelea, ingawa wadadisi wa mambo wanaona China inaiunga mkono Moscow.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.