Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Ujerumani: Watu kadhaa wauawa kwa kupigwa risasi katika kituo cha Mashahidi wa Yehova Hamburg

Risasi zilifyatuliwa Alhamisi jioni, Machi 9, katika kanisa la waumini wa kanisa la Mashahidi wa Yehova katika wilaya ya Gross Borstel huko Hamburg, jiji la bandari kaskazini mwa Ujerumani.

Maafisa wa polisi wakiwasili huko Hamburg katika eneo la tukio liliotokea kanisani katika wilaya ya Gross Borstel, Machi 9, 2023 jioni.
Maafisa wa polisi wakiwasili huko Hamburg katika eneo la tukio liliotokea kanisani katika wilaya ya Gross Borstel, Machi 9, 2023 jioni. © AP - Jonas Walzberg
Matangazo ya kibiashara

Watu kadhaa waliuawa na wengine kujeruhiwa vibaya. Polisi bado haijatoa idadi kamili, lakini gazeti la kila siku la Bild linazungumzia watu saba waliofariki na wanane kujeruhiwa. Kulingana na msemaji wa polisi, mhusika wa tukio hili anaweza kuwa miongoni mwa waliofariki.

Tukio hili lilitokea katika kituo kilichowaleta pamoja waumini wa kanisa la Mashahidi wa Yehova kaskazini mwa jiji la Hamburg, jioni ya Alhamisi, Machi 9. Walikuwa wamekusanyika saa moja usiku kwa ajili ya mkutano wa kila wiki wa funzo la Biblia, llinaripoti gazeti la kila siku la Hamburger Abendblatt.

"Karibu saa tatu usiku, mtu mmoja au zaidi wasiojulikana waliwafyatulia watu risasi," Ofisi ya Shirikisho ya Ulinzi wa Raia ilisema, ambayo ilionya katika taarifa: "Epukeni eneo la hatari. Katika eneo la hatari, kaeni hapo mlipo na msitoke nje kwa sasa. "

Msemaji wa polisi amekiambia kituo cha televiseni cha NTV kwamba vikosi vya usalama "waliitwa mwendo wa saa tatu na dakika kumi na tano usiku wakiambiwa kuhusu tukio hili la shambulizi kwenye jengo hilo", lililoko katika wilaya ya Gross Borstel. "Waliingia ndani ya jengo hilo haraka sana na kukuta watu wameuawa na kujeruhiwa vibaya".

Ulinzi wa kituo hicho bado unaendelea, polisi hawajatoa, kufikia sasa, idadi kamili ya waathitiriwa. Lakini gazeti maarufu la kila siku la Bild, ambalo limetaja tukio hili kama la 'umwagaji damu', linaripoti idadi ya awali ya watu saba waliofariki na wanane kujeruhiwa vibaya.

Mshambuliaji anaaminika kuwa miongoni mwa waliouawa

Katika Twitter, polisi wa Hamburg ilisema kwamba "idadi kubwa ya maafisa wa polisi wako katika eneo la tukio". Kulingana na vyombo vya habari kadhaa, wakazi wa jiji la bandari walionywa kuhusu "hatari kubwa" kupitia Appli ya tahadhari ya majanga, polisi wakiwataka eneo husika.

Mhusika wa tukio hili anaweza kuwa miongoni mwa waliofariki, polisi katika mji wa bandari wa kaskazini mwa Ujerumani imesema. Kuna "viashiria kwamba mhalifu anaweza kuwa ndani ya jengo hilo, ikiwezekana hata miongoni mwa waliofariki," msemaji wa polisi ameiambia televisheni ya NTV.

Kwenye Twitter, Meya wa Hamburg Peter Tschentscher amesela: "Habari kutoka kwa Alsterdorf/Gross Borstel ni za kuhuzunisha. Vikosi vya usalama vinafanya kazi bila kuchoka kuwafuatilia wahusika na kubaini mazingira ya tukio hili . "

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.