Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Ujerumani: Mhusika wa shambulio katika Kanisa la Mashahidi wa Yehova ni muumini wa zamani

Polisi ya Ujerumani bado haijajua sababu ya shambulio dhidi ya kanisa la Mashahidi wa Yehova mnamo Alhamisi, Machi 9, huko Hamburg, ambalo liliua watu wanane. Mhusika mkuu wa shambulio hili ni muumini wa zamani wa kanisa hilo, ambaye pia alijiua, baada ya kuwafyatulia risasi waumini wenzake.

Nje ya jengo la Mashahidi wa Yehova huko Hamburg, Ujerumani, Ijumaa, Machi 10, 2023.
Nje ya jengo la Mashahidi wa Yehova huko Hamburg, Ujerumani, Ijumaa, Machi 10, 2023. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Watu wanane wameuawa akiwemo mshambuliaji wa shambulio hilo na kijusi cha miezi saba. Wanane wamejeruhiwa, wanne vibaya. Hii ndiyo ripoti ya shambulizi jana usiku katika kanisa la Mashahidi wa Yehova huko Hamburg. Viongozi walikutana na kutoa idadi hii katika mkutano na waandishi wa habari. Kuwepo kwa vikosi maalum vya polisi vilivyo wekwa karibu na kanisa hili kuliweza kuzuia idadi kubwa zaidi ya watu ambao wangeliuawa.

Mhusika wa shambulio hilo alikimbilia ndani ya jengo kabla ya kujitoa uhai. Alikuwa na risasi nyingi juu yake na mamia yalipatikana nyumbani kwake. Philipp F. alikuwa na leseni halali ya kumiliki bunduki.

► Soma pia: Watu kadhaa wauawa kwa kupigwa risasi katika kituo cha Mashahidi wa Yehova Hamburg

Kuelekea mijadala mingi...

Barua isiyojulikana iliyozungumzia matatizo yake ya kisaikolojia ilipelekea, mwezi uliopita, kupimwa nyumbani kwake. Polisi hawakuamini kuwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha kufanya uchunguzi zaidi. Habari hii bila shaka itazua mijadala mingi.

Philipp F. ni mshiriki wa zamani wa jumuiya hii ya Mashahidi wa Yehova aliyoiacha mwaka mmoja na nusu uliopita. Kulingana na mamlaka, alikuwa na chuki kwa jamii hii. Nia ya kisiasa au ya kigaidi haijajumuishwa. Wachunguzi wanaweza baadaye kujifunza zaidi kuhusu nia hasa za Philipp F.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.