Pata taarifa kuu

Washington yatangaza msaada mpya wa kijeshi wa dola bilioni 2 kwa Ukraine

Washington itatoa awamu nyingine ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine, kiasi cha dola bilioni 2, mwaka mmoja baada ya kuzuka kwa uvamizi wa Urusi, afisa mkuu wa Marekani alitangaza Alhamisi.

Katika picha hii iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Ukraine, rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anasikiliza wimbo wa taifa wakati wa ziara yake huko Kherson, Ukraine, Jumatatu, Novemba 14, 2022.
Katika picha hii iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Ukraine, rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anasikiliza wimbo wa taifa wakati wa ziara yake huko Kherson, Ukraine, Jumatatu, Novemba 14, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Ni mwaka mmoja sasa tangu kuzuka kwa vita vya Ukraine, wakati nchi nyingi zikiendelea kuihtumu Urusi kufuatia uvamizi huo.

Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametumia Telegram kukumbuka miezi 12 tangu Urusi iivamie nchi yake.

Akizungumza huku picha mbalimbali zikionyesha athari za vita, Bw Zelensky amesema kumbukumbu kama hizi "zinaacha makovu makubwa katika moyo wako na roho".

Hayo yanajiri wakati shirika la ushirikiano wa mahakama la Umoja wa Ulaya, Eurojust limeanzisha kituo kipya cha kusaidia kukusanya ushahidi wa uhalifu uliofanywa nchini Ukraine, kutokana na uvamizi wa Urusi.

Eurojust yenye makao yake mjini The Hague, imetoa tangazo hilo siku ya Alhamisi wakati ambapo jumuia ya kimataifa imekuwa ikitoa wito wa kuwawajibisha wanaohusika na uhalifu wa kivita nchini Ukraine na kufunguliwa mashtaka, baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.