Pata taarifa kuu

Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg hataki kurefusha muda wake

Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO, imefahamisha kuwa, kiongozi wake wa muda mrefu Jens Stoltenberg hana mpango wa kuongeza muda wake wa uongozi kwa mara ya nne na anatarajia kuachia nafasi hiyo mwezi Oktoba mwaka huu.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg hataki kuongeza muda wake, msemaji wa Muungano wa Atlantic alitangaza Jumapili Februari 12.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg hataki kuongeza muda wake, msemaji wa Muungano wa Atlantic alitangaza Jumapili Februari 12. REUTERS - YVES HERMAN
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo lililotolewa Jumapili hii, Februari 12 na msemaji wa Muungano wa Atlantic, linazua maswali mengi kuhusu mrithi wa katibu mkuu wa NATO katika mazingira yanayotawaliwa na vita vya Ukraine.

Kurefusha muda wa makatibu wakuu ni tabia katika NATO na Jens Stoltenberg tayari ameongezwa mara tatu. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka jana kwani tayari alikuwa amepanga kuondoka Oktoba 1, 2022. Mwaka mmoja uliopita, serikali ya Norway ilitangaza rasmi kwamba nia yake ya kuwa mkuu wa Benki ya Kitaifa ya Norway imekubaliwa. Lakini hatimaye alibadili kauli na kufutilia mbali wadhifa huo, anakumbusha mwandishi wetu wa Brussels, Pierre Benazet.

Kwa sababu ya vita vya Ukraine, washirika 30 wa NATO walikataa kubadilisha katibu mkuu katikati ya vita. Kwa hivyo waliongeza mamlaka yake kwa mwaka mmoja, hasa kwani Jens Stoltenberg, ambaye atakuwa na umri wa miaka 64 mnamo Machi, ni alikubaliana na hilo.

Kiongozi huyo wa Norway aliteuliwa kwenye wadhifa wa Katibu mkuu wa NATO mwaka 2014 wakati Urusi ilikuwa imetwaa tu Crimea na anaweza kujivunia maisha marefu ya kuhudumu kwenye wadhifa huo, kwani atakuwa amehudumu kwa miaka tisa. Kati ya Makatibu Wakuu kumi na watano waliotangulia wa NATO, ni mmoja tu aliyehudumu muda mrefu zaidi na alihudumu kwa miaka kumi na miwili.

 Mzozo wa kidiplomasia

Katikati ya vita vya Ukraine, NATO itasita kumwachilia Jens Stoltenberg na badala yake kuna hatari ya kuzusha mzozo mkubwa wa kidiplomasia, hasa kwa vile hakuna utaratibu rasmi wa kumteua Katibu Mkuu wa NATO.

Gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag lilitaja Jumapili hii kusogezwa mbele kwa miezi sita hadi mwisho wa mwezi Machi na muda huu hauwezi kuwa wa kubahatisha. Inaweza kuendana na tarehe ambapo mrithi halali anaweza kupatikana, labda mwanamke na kwa vyovyote vile labda mkuu wa zamani wa serikali. Nafasi ya katibu mkuu kawaida huangukia kwa mtuu kutoka Ulaya, kwa sababu mkuu wa kijeshi wa NATO, mkuu wa kamandi kuu ya washirika huko Ulaya, ni Mmarekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.