Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu 25,000 wafariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria

Zaidi ya watu 25,000 walifariki dunia katika tetemeko la ardhi lililokumba Uturuki na Syria siku ya Jumatatu, kulingana na ripoti rasmi za hivi punde zilizotolewa Jumamosi Februari 11.

Mtu mmoja akipita karibu na jengo lililoporomoka kufuatia tetemeko mbaya la ardhi, huko Pazarcik, Uturuki, Februari 9, 2023.
Mtu mmoja akipita karibu na jengo lililoporomoka kufuatia tetemeko mbaya la ardhi, huko Pazarcik, Uturuki, Februari 9, 2023. REUTERS - SUHAIB SALEM
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, akizuru mji wa Sianlurfa (kusini-mashariki), miili 21,848 imepatikana katika hatua hii nchini Uturuki, wakati mamlaka imehesabu watu 3,553 ambao walifariki nchini Syria.

Nchini Uturuki pekee watu wapatao 21,000 wamekufa na wengine zaidi ya 80,000 wamejeruhiwa.Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa taarifa hiyo kwenye jimbo la Diyarbakir lililokumbwa na maafa hayo.

Watu wapatao 102,000 wameshahamishwa na kupelekwa sehemu nyingine baada makaazi yao kukumbwa na maafa. Vikosi vya  waokoaji karibu 166,000 vinaendelea na juhudi za uokozi ikiwa pamoja  na waokoaji kutoka nje.

Wakati huo huo Rais Tayyip Erdogan amesema idara husika zilipaswa kufanya haraka ili kuwasaida wahanga. Rais huyo ameahidi kuanza kazi haraka kwa ajili  ya ujenzi mpya lakini pia amewaonya wahalifu wanaopora mali za watu wakati huu wa maafa.

Misaada pia imewasili nchini Syria licha ya kuwa ya kiwango cha chini kutokana na athari za vita vya muda mrefu.Shughuli za kupeleka misada hiyo zinatatizika hata baada ya serikali ya nchi hiyo kusema mapema wiki hii kwamba itaruhusu misaada kupelekwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.