Pata taarifa kuu

Tetemeko la Ardhi: UN waomba fedha kusaidia watu 874,000 nchini Uturuki na Syria

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), shirika lililobobea la Umoja wa Mataifa, limeomba dola milioni 77 kusaidia watu 874,000 walioathiriwa na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria.

Watu wamesimama kwenye vifusi huku kazi ya kuwatafuta walionusurika ikiendelea, kufuatia tetemeko la ardhi, huko Aleppo, Syria, Februari 9, 2023.
Watu wamesimama kwenye vifusi huku kazi ya kuwatafuta walionusurika ikiendelea, kufuatia tetemeko la ardhi, huko Aleppo, Syria, Februari 9, 2023. REUTERS - FIRAS MAKDESI
Matangazo ya kibiashara

"WFP inaomba dola milioni 77 kutoa msaada wa mgao wa chakula na vyakula vya moto kwa jumla ya watu 874,000 walioathiriwa na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria," shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Roma limesema.

Siku nne baada ya mkasa huo mbaya, miujiza bado inaonekana kwa baadhi ya watu kuokolewa wakiwa hai kutoka chini ya vifusi. Katika mji wa Antakya, msichana wa miaka 10 ameokolewa usiku wa leo akiwa hai. Katika jimbo la Hatay nchini Uturuki, watu 9 wamegundulika kuwa hai baada ya kukwama kwenye jengo kwa muda wote.

Hayo yanajiri wakati msaada wa kwanza wa Umoja wa Mataifa ulifanikiwa kuwasili siku ya Alhamisi katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi nchini Syria lakini matumaini ya kuwapata manusura zaidi yamefifia tangu zipite siku tatu ambazo wataalamu wanazingatia kama kipindi muhimu cha kuokoa maisha ya binadamu. 

Msafara wa Umoja wa Mataifa uliobeba misaada ulivuka mpaka wa Uturuki na kuingia eneo la Kaskazini Magharibi mwa Syria linaloshikiliwa na waasi, ikiwa ndio njia pekee ya kuwafikia raia bila ya kupitia maeneo yanayothibitiwa na vikosi vya serikali ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.