Pata taarifa kuu
UTURUKI- SYRIA

Uturuki,Syria :Idadi ya watu waliofariki kwa tetemeko la ardhi imefikia zaidi ya watu elfu 21

KENYA – Idadi ya watu waliofariki katika tetemeko la ardhi lililoikumba Uturuki na Syria, imeongezeka na kufikia elfu 21, wakati huu msaada wa kwanza wa umoja wa mataifa ikiwasili kaskazini magharibi mwa Syria.

Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Syria na Uturuki imendelea kuongezeka.
Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Syria na Uturuki imendelea kuongezeka. © Sertac Kayar / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kulinganana mamlaka za uokoaji idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka, wakati huu hali ya baridi kali nchini Uturuki ikionekana kulemaza shughuli za uokoaji na kutishia maisha ya maelfu ya manusura waliopoteza makazi yao.

Wakati huu juhudi za uokoaji zikiendelea, makumi kwa maelfu ya manusura wa mkasa huo wamehamishwa kutoka katika miji nchoini Uturuki ilioathirika zaidi, huku raia katika miji nchini Syria wakisaidia kuwazika wenzao waliopoteza maisha.

Katika hatua nyingine, mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa muda ambao umoja wa mataifa ulichukuwa kutuma msaada Kaskazini Magharibi mwa Syria, wakati huu mataifa kadhaa yakiwemo China na Marekani yakiahidi kutoa msaada zaidi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.