NATO: Nchi wanachama zitaendelea kushirikiana na Japan
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, Jens Stoltenberg, amesema nchi wanachama zitaendelea kushirikiana na Japan, hasa wakati huu ambao usalama wan chi zao unatishiwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Imechapishwa:
Cheza - 00:28
Stoltenberg, amesema ziara yake kwenye miji ya Tokyo na Seuol, Korea Kusini, inalenga kuimarisha ushirikiano wa kijeshi baina ya nchi hizo, na kwamba watahakikisha dunia inaendelea kuwa salama.
“Vita nchini Ukraine vinatuonyesha kuwa usalama wetu kwa pamoja unategemeana.”ameeleza Jens Stoltenberg.
Mataifa wanachama wa NATO wamekuwa wakitoa wito wa kushirikiana ilikupambana na kile wanachosema ni tishio la dunia kutoka kwa mataifa kama Urusi na Korea kaskazini.