Pata taarifa kuu

Ukraine: Zelensky aahidi kutoa 'vifaa vinavyohitajika' kwa askari wake Bakhmout na Soledar

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameahidi Alhamisi Januari 12 kutoa "kila kitu kinachohitajika" katika suala la vifaa kwa wanajeshi wanaopinga mashambulizi ya Urusi huko Bakhmout na Soledar, miji miwili mashariki mwa nchi hiyo ilio chini ya shinikizo kutoka kwa vikosi vya Moscow.

Rais Zelensky amesema Urusi na washirika wake wanajaribu kueneza propaganda kwa madai ya kuukamata mji huo lakini ukweli ni kwamba mapambano bado yanaendelea.
Rais Zelensky amesema Urusi na washirika wake wanajaribu kueneza propaganda kwa madai ya kuukamata mji huo lakini ukweli ni kwamba mapambano bado yanaendelea. © AP/Carolyn Kaster
Matangazo ya kibiashara

"Ninataka kusisitiza kwamba wanajeshi wanaotetea miji hii watapewa risasi na kila kitu kinachohitajika kwa njia ya haraka na isiyokatizwa," Voodomyr Zelensky amesema kwenye Facebook baada ya mkutano na maafisa wakuu katika makao makuu ya jeshi.

Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mapigano bado yanaendelea katika mji muhimu wa mashariki mwa nchi hiyo wa Soledar ambao mamluki wa kundi binafsi la ulinzi kutoka Urusi la Wagner wamesema wameukamata. 

Rais Zelensky amesema Urusi na washirika wake wanajaribu kueneza propaganda kwa madai ya kuukamata mji huo lakini ukweli ni kwamba mapambano bado yanaendelea. Pande zote mbili Urusi na Ukraine zimesema mapigano ya kuwania udhibiti wa mji huo ni makali na yamechukua muda mrefu huku Moscow ikitahadharisha kuhusu madai ya ushindi wa mapema yanayotolewa na kundi la Wagner. 

Mji wa Soledar ulioko mkoa wa Donetsk na unaofahamika kwa uzalishaji mkubwa wa chumvi, unapatikana kiasi maili tisa kutoka mji mwingine wa Bakhmut ambao vikosi vya Urusi vimekuwa vikijaribu pia kuukamata.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.