Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Urusi yafanya mashambulizi Kherson, Zelensky alaani kitendo cha 'ugaidi'

Nchini Ukraine kunaripotiwa matukio ya kutisha, hasa katika jimbo la Kherson, baada ya mashambulizi ya angani Jumamosi asubuhi, Desemba 24, katika eneo la kibiashara katikati mwa jiji. Kulingana na ripoti ya kwanza ya awali, mashambulizi ya angani yamesababisha vifo vya watu 7 na wengine 58 kujeruhiwa, ripoti ambayo itakuwa mbaya zaidi katika saa zijazo.

Magari yakiteketea kwa moto baada ya shaambulizi la Urusi katika jiji la Kherson, Desemba 24, 2022.
Magari yakiteketea kwa moto baada ya shaambulizi la Urusi katika jiji la Kherson, Desemba 24, 2022. © Ukrainian Presidential Press Service/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi asubuhi, eneo la maduka katikati mwa jiji la Kherson, likiwemo soko lililofunikwa na duka kubwa vimekumbwa na mashambuliozi ya angani. Makombora kadhaa, ambayo onadaiwa kuwa yalirushwa na silaha kubwa inayorusha makombora mengi ya aina ya Grad, yalilipuka ardhini na kwenye majengo ya soko kuu, yakipunguza idadi ya wapita njia, ambao walikuwa wengi sana wakati huo.

Picha za kwanza ni za baridi: karibu na maduka, miili kadhaa ya watu waliouawa imegunduliwa kwenye madimbwi ya damu, na watu wengine kadhaa wamejeruhiwa, baadhi wakiwa katika hali mbaya.

Kherson, yakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara

"Mkesha wa Krismasi, katikati mwa jiji, sio vita kwa sheria zilizowekwa. Ni ugaidi, ni mauaji ya kutisha na ya kujifurahisha," Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alikashifu mara moja kwenye mitandao ya kijamii. Baada ya kukombolewa mnamo Novemba 11 na jeshi la Ukraine baada ya kukaliwa kwa miezi tisa, Kherson tangu wakati huo inalengwa mara kwa mara na mashambulizi ya angani ya Urusi. 

Katika muktadha huu, utawala wa kijeshi wa kiraia wa Kherson umewataka wakaazi karibu na kingo za Mto Dnieper kuuhama mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.