Pata taarifa kuu

Bei ya nishati: Emmanuel Macron aunga mkono utaratibu wa mchango wa Ulaya

Hatimaye rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekubaliana na fikra ya kuanzisha utaratibu wa pamoja kuhusiana na mchango wa Ulaya katika kukabiliana na bei ya nishati barani humo.

Rais wa Ufaransa akiambatana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz wamefanya mkutano na waandishi wa habari huko Élysée mnamo Septemba 5, 2022.
Rais wa Ufaransa akiambatana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz wamefanya mkutano na waandishi wa habari huko Élysée mnamo Septemba 5, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano Septemba 5, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alielezea kwa kirefu mkakati wa Ufaransa na Ulaya wa kukabiliana na mgogoro wa nishati. Pia aligusia suala nyeti la bei, na utaratibu wa mchango wa Ulaya kwa makampuni ya nishati wanaopata faida kubwa. 

Siku ya Jumatatu Ufaransa ilisema kwamba inaunga mkono Umoja wa Ulaya kuweka mchango kwa makampuni ya nishati ambayo yatapata "faida isiyofaa" na kuongezeka kwa bei ya jumla ya umeme katika bara la Ulaya, ikiungana na Ujerumani ambayo ilipendekeza mbinu hii, Jumapili 4 Septemba. "Tunatetea utaratibu wa uchangiaji wa Ulaya (...) ambao kwa hivyo utaombwa kutoka kwa makampuni yanishati", alitangaza Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati Tume ya Ulaya inatayarisha mpango wake wa kudhibiti kupanda kwa bei ya umemeiliyoshuhudiwa katika majira ya Joto.

Zaidi ya yote, msiseme "kodi kwa faida kubwa". Lakini kwa kubainisha faida "zisizofaa", "zinazozidi" za makampuni ya nishati, ambayo "gharama za uzalishaji ni za chini sana kuliko bei ya sokoni", Emmanuel Macron alitoa ufafanuzi kamili. Hata hivyo, kambi ya rais haioni mabadiliko au makubaliano. "Serikali, Rais wa Jamhuri, Waziri wa Uchumi kwa wiki nyingi wamependekeza mageuzi ya soko la nishati la Ulaya. Kwa hivyo, ninaamini kuwa matamshi ya rais yanafafanua na kukamilisha mbinu hii, "alisema David Amiel, Mbunge kutoka chama cha Renaissance na mwandishi mwenza wa misheni ya bunge kuhusu mada hiyo.

Utaratibu usio wa kifedha

Badala ya kodi ya kitaifa kwa "faida kubwa", Ufaransa inaunga mkono utaratibu katika ngazi ya Ulaya, ambayo ingewezesha kurejesha sehemu ya faida inayotolewa na makampuni ya nishati. Berlin imeahidi kuunga mkono aina hii ya utaratibu na Tume. Chombo hiki kitatumika kwa kampuni zinazozalisha umeme katika mitambo ya nyuklia, makaa ya mawe au kutoka kwa vyanzo vinavyoweza kurejeshwa. Makampuni haya sasa yananufaika kutokana na kupanda kwa bei ya umeme katika bara la Ulaya, iliyoshushwa baada ya gesi. Bei ya umeme ya Ulaya kwa kweli imeorodheshwa kwa ile ya gesi, ambayo imefikia urefu wa kihistoria tangu vita vya Ukraine. Bei za umeme zilivunja rekodi mpya, kwa euro 1,000 kwa megawati moja kwa saa, dhidi ya euro 85 mwaka mmoja uliopita. Hii ndiyo sababu Ufaransa inadai kutoka Brussels mageuzi ya haraka ya mfumo ili kuzuia kupanda kwa umeme ambao unakuza mfumuko wa bei.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.