Pata taarifa kuu

Ufaransa: Emmanuel Macron atetea jibu la Ulaya kwa mgogoro wa nishati

Baada ya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Emmanuel Macron ametetea Jumatatu hii, Septemba 5, jibu la Ulaya kwa mgogoro wa sasa wa nishati. Hasa amependelea mageuzi ya bei ya umeme na kufungua mlango wa mchango wa kipekee wa kifedha kutoka kwa baadhi ya makampuni katika sekta hiyo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba baada ya mkutano na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwa njia ya video kuhusu mgogoro wa nishati, kwenye Ikulu ya Elysée huko Paris, Jumatatu, Septemba 5, 2022.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba baada ya mkutano na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwa njia ya video kuhusu mgogoro wa nishati, kwenye Ikulu ya Elysée huko Paris, Jumatatu, Septemba 5, 2022. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwa njia ya video, kuhusu hali ya nishati barani Ulaya, rais wa Ufaransa amefanya mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Elysee siku ya Jumatatu. Ametangaza kwamba Ufaransa itaongeza uwezo wake wa kusafirisha gesi kwa Ujerumani na kwamba nchi hiyo imekubali kupeleka umeme kwa Ufaransa ikiwa itahitajika.

Katika ngazi ya Ulaya, "tunapendelea mazoea ya kawaida ya ununuzi wa gesi", ameelezea rais wa Ufaransa wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Aidha, "kama Tume ingeamua kuweka ukomo wa bei ya gesi iliyonunuliwa kupitia mabomba ya gesi kutoka Urusi, Ufaransa ingeunga mkono hatua hiyo", ameongeza.

Pia ametetea kanuni ya "utaratibu wa mchango wa Ulaya" kwa wadau wa nishati "mchango ambao gharama za uzalishaji ni chini sana kuliko bei ya uuzaji kwenye soko", akimaanisha "faida isiyofaa". Mchango huu, ameeleza, unaweza kurejeshwa kwa nchi wanachama ili kufadhili hatua za kitaifa.

Rais wa Ufaransa pia amesema kwamba "bei (ya umeme) lazima iwekwe kwa njia thabiti zaidi" na akapendekeza kuongezeka kwa mapambano dhidi ya mazoea ya kubahatisha kwenye soko la nishati.

Tayari mzozo wa nishati barani Ulaya umechukua hatua mpya siku ya Ijumaa na tangazo la kampuni ya gesi ya Urusi ya Gazprom la kusitisha uwasilishaji wake kwa muda usiojulikana kupitia bomba la gesi la Nord Stream 1, ambalo linahudumia nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ujerumani.

Emmanuel Macron pia alionyesha upinzani wake thabiti kwa kuzinduliwa upya kwa mradi wa bomba la gesi la MidCat (Midi-Catalonia) katika muktadha wa mvutano wa nishati unaohusishwa na mzozo wa Ukraine, akibaini kwamba haukujibu masuala ya sasa.

Hata hivyo, ameongeza, ikiwa Olaf Scholz au Rais wa Uhispania Pedro Sanchez wangemuonyesha kinyume chake, "niko tayari kuhakiki msimamo wangu".

Uhispania na Ureno zina uwezo mkubwa wa kuagiza gesi na Kansela wa Ujerumani, hasa, alipendekeza tena mnamo Agosti chaguo la MidCat kuboresha miunganisho ya mtandao wa gesi huko Ulaya. Ufaransa imekuwa ikipinga hili kwa muda mrefu, ikitaja hasa gharama ya mradi huo, na kupendelea uwekaji wa vituo vipya vya LNG.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.