Pata taarifa kuu

Ufaransa: Baraza la Ulinzi la Nishati lawataka Wafaransa kujipanga

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameitisha kikao cha Baraza la Ulinzi siku ya Ijumaa, Septemba 2, kuhusu mgogoro wa nishati. Lengo ni kuchunguza matukio tofauti ili kuandaa serikali kwa hali zote zinazoweza kutokea wakati wa majira ya baridi, na kuepuka mgawo au kupunguzwa kwa umeme. Hakukuwa na tangazo madhubuti mwishoni mwa kikao hiki cha Baraza wa Nisahti, lakini lengo lilikuwa juu ya yote kueleza "usawa" unajumuisha nini na kuwahakikishia Wafaransa.

Waziri Mkuu, Elisabeth Borne, na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, walipiga picha hapa wakati wa maadhimisho ya miaka 82 kwa wito wa Jenerali De Gaulle, Juni 18, 2022.
Waziri Mkuu, Elisabeth Borne, na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, walipiga picha hapa wakati wa maadhimisho ya miaka 82 kwa wito wa Jenerali De Gaulle, Juni 18, 2022. AP - Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Wazo ni kuwaambia Wafaransa kwamba "ikiwa tutajipanga, tutamaliza msimu wa baridi bila tatizo lolote", ameelezea mjumbe wa serikali kwa kuzungumza kwa muhtasari kuhusu lengo la kikao cha Baraza hili la Ulinzi wa Nishati.

"Ili kuepusha mabaya zaidi, lazima tujitayarishe kwa hilo. "Mawasiliano ambayo yanabadilisha hotuba ya kutisha ya Emmanuel Macron. Tangu kuanza kwa mwaka wa shule, rais ameelezea kuwa "wingi" na "uzembe" vimekwisha.

Kwa kuchagua muundo wa Baraza la Ulinzi, Emmanuel Macron alitaka kuonyesha hatari ya mgogoo huu, lakini pia kusema kwamba uko chini ya udhibiti.

Serikali pia inataka kuepuka kutoa masomo kwa Wafaransa. Zaidi ya yote, inataka kutoa wto kwa wajibu wao wa kupunguza joto, kuzima taa na kushiriki katika jitihada za pamoja.

Waziri wa Mpito wa Nishati, Agnès Pannier Runacher, pia ametangaza kuwa bei ya umeme itaendelea kulipwa kwa sehemu na kwamba Ufaransa imeunda akiba ya gesi ya hadi 92% ya uwezo wake.

Kutokana na mlipuko wa bei za umeme na gesi, makampuni tayari yanalazimika kupunguza uzalishaji wao. 
Katika Duralex, tanuri ya kiwanda hivi karibuni itawekwa kwenye hali ya kusubiri.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.