Pata taarifa kuu

Ujerumani kutoa euro bilioni 65 kwa ajili ya nguvu ya ununuzi

Ujerumani itatoa euro bilioni 65 kufadhili mpango wake mpya wa msaada unaonuiwa kuwalinda watumiaji na wafanyabiashara kutokana na athari za mfumuko wa bei unaoongezeka. Mpango huo umeidhinishwa siku ya Jumapili na pande tatu za serikali ya mseto ya Kansela Olaf Scholz.

Olaf Scholz amezindua mfululizo wa hatua, ikiwa ni pamoja na hundi ya mara moja ya nishati ya euro 300 kwa mamilioni ya wastaafu na euro 200 kwa wanafunzi.
Olaf Scholz amezindua mfululizo wa hatua, ikiwa ni pamoja na hundi ya mara moja ya nishati ya euro 300 kwa mamilioni ya wastaafu na euro 200 kwa wanafunzi. REUTERS - CHRISTIAN MANG
Matangazo ya kibiashara

Mpango mkubwa wa msaada kwa nguvu ya ununuzi. Serikali ya Ujerumani ilitangaza, Jumapili, Septemba 4, hatua nyingi za kupunguza athari za mfumuko wa bei wa euro bilioni 65 na baada ya majadiliano magumu ndani ya muungano wa Olaf Scholz.

Chama cha Social Democrat, kikiongoza muungano ulioundwa na wanamazingira na waliberali, wamekusanya siku ya Jumamosi, hadi jioni, vongozi wakuu wa serikali ili kukamilisha mpango huu, ambao ulikuwa unasubiriwa kwa wiki kadhaa.

Akirudia msemo wake kwamba Wajerumani "hawatawahi kuwa peke yao" katika kukabiliana na tatizo la nishati, Olaf Scholz amezindua mfululizo wa hatua, ikiwa ni pamoja na hundi ya mara moja ya nishati ya euro 300 kwa mamilioni ya wastaafu na euro 200 kwa wanafunzi.

Mfumuko wa bei uliongezeka tena nchini Ujerumani mnamo Agosti, hadi 7.9% kwa mwaka mmoja, bado unasababishwa na kupanda kwa bei ya nishati kutokana na vita vya Ukraine.

Mnamo mwezi Oktoba, ushuru wa gesi unaokusudiwa kuzuia kufilisika kwa mashirika ya nishati ya Ujerumani lazima uanze kutumika. Itasababisha kuongezeka zaidi kwa muswada wa nishati.

Mkuu wa benki kuu ya Ujerumani, Bundesbank, ameona kuna uwezekano kwamba mfumuko wa bei utafikia 10% ifikapo mwisho wa mwaka, ikiwa ni mara ya kwanza tangu miaka ya 1950.

Kulenga 'uvumi'

Kama ilivyo katika nchi zingine za Ulaya, kupanda kwa bei kunachochea wasiwasi wa umma na wito wa maandamano, hasa kwa mrengo wa kulia au kushoto kabisa, unaitia wasiwasi serikali.

Tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwishoni mwa mwezi wa Februari, serikali ya Olaf Scholz tayari imetoa treni mbili za msaada kwa kaya zenye jumla ya euro bilioni 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.