Pata taarifa kuu
ULAYA- JOTO

Uingereza, Ufaransa kuendelea kushuhudia viwango vya juu vya joto

Nchi za Uingereza na Ufaransa, hivi leo zimeshuhudia kiwango cha juu cha joto, wakati huu raia kwenye maeneo ya kusini magharibi mwa bara la Ulaya wakishuhudia ongezeko la joto na moto wa nyika unaounguza misitu.

Baadhi ya wakazi wa jiji la paris wakijikinga na joto kando la chemichemi ya maji nchini Ufaransa.
Baadhi ya wakazi wa jiji la paris wakijikinga na joto kando la chemichemi ya maji nchini Ufaransa. AFP - STEFANO RELLANDINI
Matangazo ya kibiashara

Wataalamu wa hali ya hewa nchini Uingereza, jote litafikia nyuzijoto 40 kwa mara ya kwanza kuanzia hivi leo na siku zijazo, hali iliyosababisha mamlaka kutangaza dharura kukabiliana na hali hiyo.

Haya yakijiri, nchini Ufaransa vikosi vya zima moto kwa siku kadhaa sasa tangu juma lililopita, vimekuwa vikikabiliana na moto wa nyika uliounguza hekari kadhaa za misitu kwenye miji ya kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Baadhi ya miji kwenye nchi za Ufaransa, Ureno, Hispania na Ugiriki, ikitarajiwa kurekodi nyuzijoto 42.

Wataalamu wakihusisha yanayotokea barani Ulaya na athari za mabadiliko ya tabia nchi, wakionya kuwa huenda hali ikazidi kuwa mbaya zaidi siku za usoni ikiwa hatua stahiki hazitachukuliwa na viongozi wadunia kudhibiti hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.