Pata taarifa kuu
UFRANSA- JOTO

Ufaransa: Raia 16,000 wameondolewa katika maeneo yanayoweza kauthirika na moto

Serikali ya Ufaransa imelazimika kuwaondoa raia zaidi ya 16, 000 katika makaazi yao kusini Magharibi mwa taifa hilo, wakati huu moto unaotokana na joto kali ukiendelea kuenea katika mataifa ya Hispania na ugiriki.

Watoto wakijikinga na joto jijini Paris siku ya Ijuma
Watoto wakijikinga na joto jijini Paris siku ya Ijuma REUTERS/Regis Duvignau
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Ufaransa katika eneo la Kitali la Gironde, yamesema yamewondoa raia kutoka maeneo ambayo yanaweza atharika na moto ambao unasambaa kwa kasi, maeneo ya Teste-de-Buch na Landiras yakiwa tayari yameathirika.

Nchini Hispania watu 3200, wamekimbia makwao katika maeneo ya Mijas, kutokana na kusambaa kwa moto huo, huku watu 1, 000 wakiripotiwa kufariki nchini Ureno na Hispani kutoka na moto.

Aidha zaidi ya ekari 75,000 za shamba nchini Ureno zimeharibiwa na moto mwaka huu kaskazini mwa taifa hilo.

Wazima moto na ndege za kuzima moto wanaendeleza shughuli ya kuzima moto eneo lote la Mediterranean, tangu juma lililopita, eneo nzima likishuhudia joto la nyuzi za juu, hali hii ikihusishwa pakubwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Mapema Jumamosi, Ufaransa iliyaweka zaidi ya maeneo 22 katika tahadhari ya juu haswa katika maeneo ya pwani mwa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.