Pata taarifa kuu
ULAYA- AFYA

EU: Imependekeza dozi ya pili ya uviko 19 kwa raia wenye umri wa miaka 60 na zaidi.

Kitengo kinachohusika na maswala ya afya katika umoja wa ulaya EU, kinapendekeza kuchomwa kwa dozi ya pili ya chanjo ya uviko 19 kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 60 pendekezo linalokuja wakati huu maambukizi yakiripotiwa kupanda.

CHANJO YA UVIKO 19
CHANJO YA UVIKO 19 AFP - JUSTIN TALLIS
Matangazo ya kibiashara

Stella Kyriakides, kamishena anayehusika na maswala ya afya na ubora wa chakula katika tume ya umoja wa ulaya ameeleza kuwa hatua hii vile vile inatokana na idadi ya watu wanaolazwa hosipitalini wakati huu msimu wa baridi unapokaribia.

 

Kitengo hicho aidha kimekuwa kikiwahimiza watu walio na umri wa miaka 80 kuchoma chanjo ya pili au ya nne tangu mwezi Aprili. Kyriakides, akitoa wito kwa mataifa yalio chini ya mwavuli wa EU kuzindua zoezi la kutoa chanjo kwa watu walio na umri wa miaka 60 kwa haraka ilikuwakinga kutokana hatari ya kuambukizwa uviko 19.

 

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO, visa vya uviko 19 vimekuwa vikipanda kwa kasi tangu mwishoni mwa mwezi mei mwaka huu katika baadhi ya mataifa ya bara ulaya.

 

Mataifa 53 yalio chini ya EU yameripoti maambukizi mapya 675,000 ya uviko 19 katika siku ya Ijuma peke.Imesema ripoti ya WHO.

 

Kuelekea mwishoni mwa mwezi Juni, Who ilikuwa imeonya mataifa ya EU kutarajiwa kushuhudia kasi ya maambukizi ya uviko 19 katika msimu huu wa baridi kutokana na uwepo wa aina mpya ya uviko 19 BA.5.

 

Aidha WHO inaeleza kuwa taifa la Cyprus linashuhudia idadi kubwa ya maambukizi ikifuatiwa na Ufaransa, Ugriki, Italia, Luxembourg na Austria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.