Pata taarifa kuu

Mataifa ya G7 kusaidia Ukraine kwa hali na mali

Mataifa ya G7 yaliyoendelea kiviwanda duniani, wameapa kuendelea kusimama na Ukraine kwa kuipa msaada kifedha na kijeshi,wakati huu inapoendelea kushambuliwa na Urusi. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Hakikisho hili, limekuja baada ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kuwahotubia viongozi hao wanaokutana nchini Ujerumani, na kuwaomba msaada zaidi wa vifaa vya kijeshi kupambana na wanajeshi wa Urusi wanaoendelea kupambana kudhibiti êneo la Mashariki mwa nchi yake. 

Aidha, rais Zelensky akiwahotubia viongozi hao wanaokutana nchini amewaambia viongozi hao kuwa angepoenda vita hivyo vimalizike kufikia mwisho wa mwaka huu. 

Mbali na kutoa hakikisho la kusimama na Ukraine, viongozi hao wa G 7 wameitaka Urusi kuacha vyakula hasa nafaka kuruhusiwa kuondoka Kiev hali ambayo imesababisha kupanda kwa bei ya bidhaa duniani. 

Wakati huo huo, viongozi hao wanatarajiwa kutangaza vikwazo vipya vya kiuchumi vinavyolenga Urusi, siku moja baada ya kutangaza mpango wa kuzuia bidhaa za Urusi kama mafuta na ghadhabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.