Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron : Ukraine italazimika kufanya mazungumzo na Urusi

Katika siku ya 112 ya uvamizi waUrusi dhidi ya Ukraine Jumatano hii Juni 15, njia salama ya kibinadamu itafunguliwa hadi saa kumi na moja jioni ili kuruhusu zoezi la kuwahamisha raia kutoka kiwanda cha Azot katika eneo la Sievierodonetsk, linalokabiliwa na mapigano.

Rais Emmanuel Macron wakati a hotuba yake katika kambi ya jeshi la anga la NATO, Juni 15, 2022.
Rais Emmanuel Macron wakati a hotuba yake katika kambi ya jeshi la anga la NATO, Juni 15, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Urusi imetangaza kuweka njia salama ya kibinadamu ili kuruhusu zoezi la kuwahamisha raia kutoka kiwanda cha Azot huko Sievierodonetsk, kwenda kijiji kinacho dhibitiwa na Urusi.

Hata hivyo Kyiv haikujibu wito wa kutaka ishushe bendera nyeuipe ili kuunhganana zoezi hili , huku rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akivitaka vikosi vyake kujizatiti vilivyo.

Mamlaka nchini Ukraine imethibitisha kwamba vikosi vya Urusi vimeharibu daraja la mwisho linaloekelea katika mji wa Sievierodonetsk, mashariki mwa Ukraine, na hivyo kuzuia njia inayotumiwa kwa kuhamisa raia waliokwama kutokana na mapigano yanayoukumba mji huo muhimu nchini Ukraine.

Emmanuel Macron  ametembelea vikosivya jeshi la Ufaransa vilivyotumwa katika kambi ya jeshi la NATO nchini Romania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.