Pata taarifa kuu

Ukraine yatangaza vifo vya wanajeshi wanne wa kujitolea wa kigeni

Jeshi la Ulinzi la Kimataifa la Ukraine, kikosi rasmi kinachosaidia vikosi vya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi , kimesema wapiganaji kutoka Ujerumani, Uholanzi, Australia na Ufaransa wamefariki, lakini hawakusema ni lini au katika mazingira gani.

Hali nchini Ukraine, Juni 3, 2022.
Hali nchini Ukraine, Juni 3, 2022. © FMM
Matangazo ya kibiashara

"Tumepoteza ndugu zetu vitani lakini ushujaa wao, utetezi wao kwa Ukraine na kujitolea kwao kwa ajili ya raia wa Ukraine vitatutia moyo milele," kikosi hiki kimesema katika taarifa.

Taarifa hiyo inaambatana na picha za watu hao, wakiwa wamejificha na wakiwa wamebeba silaha ndogo ndogo. Kwa mujibu wa tovuti ya shirika hilo, raia wa Denmark, Israel, Poland, Lithuania, Croatia, Canada na Uingereza, miongoni mwa wengine wamejiunga na vikosi vyao. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitangaza kuundwa kwa kikosi maalumu mwanzoni mwa vita, na kulingana na Kyiv, maombi 20,000 yalipokelewa. Urusi ilidai wiki hii kuwa imeua "mamia" ya wapiganaji wa kigeni nchini Ukraine tangu uvamizi wa nchi hiyo jirani kuanza Februari 24.

Kanisa moja Donetsk lateketea baada ya kukumbwa na mashambulizi

Kanisa la kihistoria huko Svyatohirsk Lavra, mkoa wa Donetsk, lililojengwa mnamo mwaka1526, lilishika moto baada ya shambulio la Urusi. "Bado hakuna hasara iliyoripotiwa, kulingana na Kanisa la Kiorthodoksi la Ukraine na afisa wa Kikosi cha Wanajeshi cha Ukraine," vyombo vya habari vya Ukraine Hromadske, ambavyo vilituma picha kwenye Twitter vimebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.