Pata taarifa kuu

Eneo la Sievierodonetsk lakabiliwa na mashambulizi makali ya Urusi

Katika siku ya 101 ya mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine, Jumamosi hii Juni 4, mashambulizi ya anga na mizinga kwa kiasi kikubwa huchangia mafanikio ya hivi karibuni ya Urusi huko Donbass, kulingana na Uingereza.

Mlipuko katika jiji la Sievierodonetsk wakati wa mapigano makali kati ya wanajeshi wa Ukraine na Urusi katika eneo la Donbass, Mei 30, 2022.
Mlipuko katika jiji la Sievierodonetsk wakati wa mapigano makali kati ya wanajeshi wa Ukraine na Urusi katika eneo la Donbass, Mei 30, 2022. AFP - ARIS MESSINIS
Matangazo ya kibiashara

Ukraine inadai kurudisha nyuma vikosi vya Urusi huko Sievierodonetsk. Wanajeshi wa Urusi walilazimishwa kurudi nyuma, Serhyi Gaïdaï, gavana wa mkoa wa Luhansk, alisema siku ya Ijumaa. "Hawakuudhibiti mji huo kikamilifu. Na kama hapo awali, tulikuwa katika hali ngumu na takriban 70% [ya jiji] lilikuwa limetekwa, kwa sasa wamerudishwa nyuma kwa 20%," alisema, licha ya mashambulizi makali.

Urusi inabaini kwamba imetimiza baadhi ya malengo ya "operesheni maalum ya kijeshi" ambayo ilizindua "kuikana" Ukraine na kulinda watu wanaozungumza Kirusi. Vita "havitakuwa na mshindi", mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini humo alisema siku ya . "Ushindi utakuwa wetu," amesema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Kusini mwa nchi, Waukraine wana wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuunganishwa kwa maeneo yaliyotekwa na majeshi ya Urusi, Moscow ikitaja kura za maoni kuhusu suala hilo kuanzia mwezi wa Julai. Lakini kwa mujibu wa amri ya kusini ya vikosi vya kijeshi vya Ukraine, Urusi imekutana na upinzani mkali sana kutoka kwa raia.

Rais wa Senegal na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Macky Sall jana alimwomba Vladimir Putin "kufahamu" kwamba Afrika imeathirika kwa mgogoro wake nchini Ukraine, kwa sababu ya hatari ya mgogoro wa chakula duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.