Malkia Elizabeth wa pili, kutohudhuria ibada ya kushukuru
Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili, anayeadhimisha miaka 70 katika nafasi hiyo, hatahudhuria ibada ya kitaifa katika Kanisa la Mtakatifu Paulo jijini London Siku ya Ijumaa , kufuatia kile kinachoelezwa kutojisikia vema kimwili.
Imechapishwa:
Hatua hii imekuja baada ya kushuhudia Gwaride na shamrashamra za kijeshi kutokea kwenye eneo la Kasri yake siku ya Alhamisi akiwa, akiwa na familia yake.
Aidha, imeelezwa kuwa uamuzi wa Malkia huyo mwenye umri wa miaka 96, kutohudhuria ibada hiyo, umefanywa kwa kusitasita kwa kuzingatia mwendo wa kuelekea Kanisani, na shughuli zitakazofuata.
Hata hivyo, siku ya Alhamisi, alishiriki kwenye hafla ya kuwasha taa.
Maadhimisho haya ya miaka sabini, yanaelezwa kuwa ya kipekee na wachambizi wa mambo wanaona huenda kusitokee kiongozi mwingine atakayekaa madarakani kwa kipindi hicho chote.
Malkia Elizabeth wa polisi, aliingia katika nafasi hiyo Juni, 2 mwaka 1953, akiwa na umri wa miaka 25, baada ya baba yake George V1 kufariki dunia.