Pata taarifa kuu

Urusi yadhibiti 'sehemu' ya Sievierodonetsk

Vikosi vya Urusi sasa vinadhibiti "sehemu" ya Sievierodonetsk, mji wa mashariki mwa Ukraine ambao wamekuwa wakishambulia kwa makombora na kujaribu kuchukua kwa wiki kadhaa, gavana wa eneo hilo ametangaza leo Jumanne.

Moshi ukifuka katika mji wa Sievierodonetsk wakati wa mapigano makali kati ya wanajeshi wa Ukraine na Urusi katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine mnamo Mei 30, 2022.
Moshi ukifuka katika mji wa Sievierodonetsk wakati wa mapigano makali kati ya wanajeshi wa Ukraine na Urusi katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine mnamo Mei 30, 2022. AFP - ARIS MESSINIS
Matangazo ya kibiashara

Ni karibu na mji huu wa Sievierodonetsk ambapo mwandishi wa habari wa Ufaransa ambaye alikuwa akifanya kazi katika kituo cha habari cha BFMTV na aliandamana na raia kwenye basi lililokuwa likibeba wakimbizi aliuawa siku ya Jumatatu.

Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Catherine Colonna, alikuwa Ukraine siku ya Jumatatu. Baada ya kusafiri hadi Bucha, alikutana na Rais Volodymyr Zelensky huko Kyiv. Alitoa wito wa kufunguliwa kwa "uchunguzi wa uwazi" juu ya kifo cha mwandishi huyo wa habari.

Viongozi wa Ulaya walifanikiwa kupata usiku wa manane kutoka Jumatatu hadi Jumanne makubaliano juu ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kwa sababu ya vita vya Ukraine. Mkataba huu unaanzishwa kwa vikwazo vya mafuta kutoka Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.