Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Moscow yadai ushindi wa eneo la Luhansk

Katika siku ya 86 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Ijumaa hii, Mei 20, majeshi ya Urusi yanaongeza shinikizo mashariki mwa Ukraine, ambapo kunaripotiza hali ,baya ya kibinada,u, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Ijumaa.

A special task force policeman inspects a site after an airstrike by Russian forces in Lysychansk, Luhansk region, Ukraine, Friday, May 13, 2022.
A special task force policeman inspects a site after an airstrike by Russian forces in Lysychansk, Luhansk region, Ukraine, Friday, May 13, 2022. AP - Leo Correa
Matangazo ya kibiashara

Mapigano yanapamba moto huko Donbass, mashariki mwa Ukraine, huku Waziri wa Ulinzi wa Urusi akisema kuwa ushindi wa eneo la Luhansk unakaribia kukamilika. Katika maeneo haya ya Sievierodonetsk na Lyssytchansk, ambayo sasa yamezingirwa wa na vikosi vya Urusi, ni ngome ya mwisho ya upinzani wa Ukraine.

"Ninamasikitiko makubwa," amesema Friday Vadim Chichimarine, mwanajeshi wa Urusi mwenye umri wa miaka 21 ambaye amefikishwa katika mahakama ya Ukraine tangu Jumatano kwa kumuua raia. Siku ya Alhamisi, upande wa mashtaka uliomba kifungo cha maisha jela. Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa siku ya Jumatatu.

Hatima ya wapiganaji wa Azovstal huko Mariupol bado haijajulikana. Urusi imeangaza Ijumaa kuwa karibu wapiganaji 2,000 wa Ukraine wamejisalimisha tangu Jumatatu. M,oja za wapiganajio wa kikosi cha Azov amesema kwenye video kwamba wanajeshi hao bado wako katika kiwanda cha chuma.

Bunge la Marekani limeidhinisha dola bilioni 40 kwa ajili ya Ukraine. Mswada huo, ambao tayari umeidhinishwa na wajumbe waliochaguliwa wa Bunge wiki iliyopita, unapaswa kuidhinishwa na Rais Biden.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.