Pata taarifa kuu

Mosco yadai kuwa wapiganaji 1,000 wa Azovstal wamejisalimisha tangu Jumatatu

Katika siku ya 84 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumatano hii, Mei 18, operesheni ya kuwahamisha wanajeshi wa mwisho wa Ukraine waliokuwa wamekimbilia katika mji wa kimkakati wa Mariupol inaendelea kulingana na Rais Volodymyr Zelensky ambaye hakutaja idadi yao.

Mabasi yaliyokuwa yamewabeba wapiganaji wa Ukraine waliojisalimisha baada ya kujificha kwa wiki kadhaa katika jengo la kiwanda cha chuma cha Azovstal yakiingia barabarani chini ya ulinzi wa jeshi la Urusi, huko Mariupol, Ukraine, Mei 17, 2022.
Mabasi yaliyokuwa yamewabeba wapiganaji wa Ukraine waliojisalimisha baada ya kujificha kwa wiki kadhaa katika jengo la kiwanda cha chuma cha Azovstal yakiingia barabarani chini ya ulinzi wa jeshi la Urusi, huko Mariupol, Ukraine, Mei 17, 2022. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Finland na Sweden kwa pamoja zimewasilisha barua zao za kuwania uenyekiti wa NATO siku ya Jumatano, nchi hizo mbili zimetangaza.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetangaza Jumatano kwamba wanajeshi 959 wa Ukraine, waliokuwa wamejificha kwenye kiwanda cha chuma cha Azovstal huko Mariupol, wamejisalimisha tangu Jumatatu. "Zoezi la kuwahamisha" askari ambao bado wako katika kiwanda cha chuma huko Azovstal "linaendelea", Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema mapema, bila kutaja idadi yao.

 Mahakama ya Ukraine inafungua kesi yake ya kwanza ya uhalifu wa kivita siku ya Jumatano kumsikiliza mwanajeshi wa Urusi anayetuhumiwa kumuua raia asiye na silaha.

 Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) alitangaza Jumanne kutumwa nchini Ukraine kwa timu ya wachunguzi na wataalam 42, ujumbe mkubwa zaidi katika masuala ya idadi kuwahi kutumwa, kuchunguza uhalifu uliofanywa wakati wa uvamizi wa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.