Pata taarifa kuu

Vita Ukraine: Kyiv yadai kuwa Urusi yasitisha mashambulizi karibu na Kharkiv

Katika siku ya 77 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumatano Mei 11, tishio la Urusi linahamia mbali na Kharkiv, mji wa pili wa Ukraine ulioko mashariki, unaokumbwa na mashambulizi tangu mwisho wa mwezi wa Februari, mamlaka ya Ukraine imesema usikuwakuaùkia Jumatano hii wakati kuna hatari mzozo kuenea kuelekea kusini magharibi kulingana na Washington.

Magari yalichomwa katika wilaya ya Saltivka huko Kharkiv, Ukraine, Mei 10, 2022.
Magari yalichomwa katika wilaya ya Saltivka huko Kharkiv, Ukraine, Mei 10, 2022. REUTERS - RICARDO MORAES
Matangazo ya kibiashara

Tishio la Urusi linaondoka Kharkiv, jiji la pili la Ukraine lililoathiriwa tangu mwisho wa mwezi wa Februari, Volodymyr Zelensky alitangaza Jumanne jioni. "Maeneo ya Cherkasy Tychky, Rusky Tychky, Rubizhne na Bayrak yamekombolewa" lakini "kiwango cha mashambulizi ya mabomu katika wilaya ya Kharkiv kimeongezeka", makao makuu ya jeshi la Ukraine imebainisha.

Vladimir Putin hana nia ya kuachana na nia yake ya kukalia kibavu eneo la Donbass nchini Ukraine pekee, lakini anataka kupeleka mzozo huo hadi Transnistria, eneo la Moldova ambalo lilijitenga mwaka 1990, mkuu wa idara ya kijasusi ya Marekani Avril Haines amesema. "Tunaamini kuwa Rais Putin anajiandaa kwa mzozo wa muda mrefu nchini Ukraine, wakati ambapo bado ana nia ya kufikia malengo zaidi ya Donbass," ameambia kikao cha bunge.

Bunge la Marekani lilichukua hatua ya kwanza Jumanne kuelekea kutolewa kwa msaada wa karibu dola bilioni 40 kwa ajili ya Ukraine, ishara aùbayo inaendelea kuonyesha uungwaji mkono wa Joe Biden kwa Kyiv. Msaada huo sasa lazima upigiwe kura katika Baraza la Seneti.

Huko Mariupol, askari "zaidi ya elfu moja " wa Ukraine, wakiwemo "mamia ya waliojeruhiwa" bado wako kwenye kiwanda cha chuma cha Azovstal kilichozingirwa na wanajeshi wa Urusi, Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.