Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Jeshi la Urusi latetea "taifa" adai Vladimir Putin

Katika siku ya 74 ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine Jumatatu hii, Mei 9, Moscow inasifia jeshi lake kwa kusherehekea ushindi dhidi ya utawala wa kinazi wa Ujerumani katika mwaka wa 1945, sherehe kubwa ili kuwatia moyo wanajeshi wake wanaokabiliwa vikali nchini Ukraine.

Kitendo cha Urusi kimekashifiwa vikali na Katibu mkuu wa umoja wa mataifa UN, Antonio Guterres ambaye anataka Moscow kutowashambulia raia wasio na hatia wakati wakati wa mapigano.
Kitendo cha Urusi kimekashifiwa vikali na Katibu mkuu wa umoja wa mataifa UN, Antonio Guterres ambaye anataka Moscow kutowashambulia raia wasio na hatia wakati wakati wa mapigano. AFP - ALEXANDER NEMENOV
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya wanajeshi wa Urusi wameandamana katika mitaa ya Moscow siku ya Jumatatu asubuhi kuadhimisha ushindi dhidi ya utawala wa kinazi  wa Ujerumani mwaka 1945. "Urusi ilikuwa inakabiliwa na tishio lisilokubalika kabisa," Vladimir Putin amesema wakati wa hotuba yake.

Watu 60 walidhaniwa kuwa wamekufa baada ya shambulio la bomu siku ya Jumamosi katika shule walimokuwa wakikimbilia katika eneo la Luhansk mashariki mwa Ukraine, ambako mapigano ya,eongewakasi, gavana wa eneo hilo Serhiy Gaïdaï alisema siku ya Jumapili.

Viongozi wa nchi za G7 waliokutana kwa njia ya video Jumapili katika mpango wa Rais wa Marekani Joe Biden wamekubali kupiga marufuku au kusitisha uagizaji wao wa mafuta ya Urusi, Ikulu ya White House ilitangaza.

"Kujisalimisha sio chaguo," wapiganaji wa mwisho waliokimbilmia katika kiwanda cha Azovstal huko Mariupol walisema Jumapili. Siku ya Jumamosi, watoto wote, wanawake na wazee waliweza kuondoka kwenye kiwandakikubwacha chuma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.