Pata taarifa kuu

Urusi kukalia majimbo kadhaa ya Ukraine

Urusi inapanga kuchukua majimbo mawili ya Ukraine eneo la Mashariki, mwa mujibu wa afisa wa juu wa Marekani, wakati huu mapamabano yakiendelea kushuhudiwa. 

Kitengo cha Kikosi cha Azov kinapiga kambi katika mkoa wa Dnipro, Ukraine, Mei 2, 2022.
Kitengo cha Kikosi cha Azov kinapiga kambi katika mkoa wa Dnipro, Ukraine, Mei 2, 2022. © Aabla Jounaïdi, RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Michael Carpenter, Balozi wa Marekani katika Shirika la ushirikiano wa usalama barani Ulaya, Urusi inampango wa kuyachukua majimbo ya Luhansk na Donetsk, ili kuwa sehemu yake mwezi huu wa Mei, kama ilivyofanya kwa Crimea mwaka 2014. 

Aidha, amesema Urusi inafikiria kuchukua jimbo lingine la Kherson, ambalo wanajeshi wake wanadhibiti n ahata sarafu yake ya Ruble kuanza kutumiwa. 

Wakati hayo yakijiri, Wizara ya Ulinzi ya Urusi, inasema watu zaidi ya Elfu 11 wakiwemo watoto Elfu Moja na mia nane, wameondolewa kutoka nchin Ukraine bila kuushirikisha uongozi wa Kiev. 

Naye Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson anatarajiwa kutangaza msaada wa Dola Milioni 400 kuisaidia Ukraine, kuendelea kupambana na Urusi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.