Pata taarifa kuu

Jeshi la Urusi lazindua mashambulizi kwenye kiwanda cha Azovstal Mariupol

Katika siku ya 69 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine Jumanne hii, Mei 3, jeshi la Urusi na watu wanaotaka kujitenga wanaounga mkono Urusi wameanzisha mashambulizi kwenye kiwanda cha Azovstal huko Mariupol, ambapo wanajeshi na raia wa Ukraine wamekimbilia.

Kiwanda cha chuma cha Azovstal, huko Mariupol, Aprili 29, 2022.
Kiwanda cha chuma cha Azovstal, huko Mariupol, Aprili 29, 2022. © AP
Matangazo ya kibiashara

► Urusi mnamo Jumanne ilianzisha shambulio dhidi ya kikosi cha mwisho cha Ukraine kinachopambana dhidi yake huko Mariupol, katika kiwanda la Azovstal.

► Vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Urusi kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine havitaondolewa hadi pale Moscow itakapofikia makubaliano ya amani na Ukraine, amesema Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, akiongeza kuwa Ukraine lazima iamue mazingira ya makubaliano haya. Mkuu wa diplomasia ya Ulaya, Josep Borrel, ametangaza kuwa vikwazo vipya viko katika maandalizi, vikilenga sekta za benki na nishati.

► Raia mia moja waliweza kuondoka katika kiwanda cha Azovstal huko Mariupol, bandari ya kusini mashariki mwa Ukraine iliyozingirwa na Urusi, siku ya Jumamosi.

► Kulingana na hesabu ya hivi punde ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi, UNHCR, zaidi ya raia 3,000 wameuawa katika mapigano na mashambulizi ya anga tangu uvamizi wa Ukraine tarehe 24 Februari.

► Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Yair Lapid Jumatatu alikashifu matamshi ya mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov, ambaye alidai kuwa Hitler "ana damu ya Kiyahudi". Mkuu wa diplomasia alikuwa akijaribu kueleza kuwa ukweli kwamba rais wa Ukraine ni Myahudi haupingani na madai ya Moscow kwamba alianzisha uvamizi huo ili "kuiangamiza" nchi.

► Urusi haitaki kumaliza vita nchini Ukraine na tarehe 9 Mei, inaadhimishwa kama siku ya ushindi, kulingana na Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.