Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Raia wa Ufaransa wajiandaa kumchagua rais

Mamilioni ya wapiga kura nchini Ufaransa, wanajiandaa kupiga kura kesho, kumchagua rais katika mzunguko wa pili, unaowakutanisha rais Emmanuel Macron na mwanasiasa wa siasa za mrengo wa kulia, Marine Le Pen.

Wagombea wa urais nchini Ufaransa Emmanuel Macron na Marine Le Pen wakiwa kwenye mdahalo wa Televisheni Aprili 20 2022
Wagombea wa urais nchini Ufaransa Emmanuel Macron na Marine Le Pen wakiwa kwenye mdahalo wa Televisheni Aprili 20 2022 © AFP / LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu  wa marudio unafanyika kwa sababu katika mzunguko wa Kwanza uliofanyika wiki mbili zilizopita na  hakuna mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura. Leo hakuna kampeni zozote zinazoendelea kote nchini.

Rais Macron anayetafuta muhula wa pili, anapewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi, baada ya wadadisi wa siasa kusema alifanya vema kwenye mjadalo wa Televisheni wiki hii dhidi ya Le Pen.

Hata hivyo, uchaguzi wa kesho pia unaelezwa kuwa na ushindani mkali kinyume na ilivyokuwa mwaka 2017, huku Marine akisema ana imani ya kuibuka mshindi licha ya sera zake, ambazo zinaonekana kuwa sio rafiki hasa barani Ulaya.

Iwapo Le Pen atashinda, atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Ufaransa, lakini pia mwanasiasa kutoka mrengo wa kulia, lakini Macron naye akifanikiwa kuchaguliwa tena, atakuwa rais wa kwanza aliye madarakani kuchaguliwa tena baada ya miaka 20.

Vituo vya kupigia kura, vitafunguliwa kuanzia mbili asubuhi saa za Paris na kufungwa baada ya saa 12 na matokeo yatafamika muda mfupi baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.