Pata taarifa kuu

Uingereza na India zatia saini ushirikiano wa ulinzi na usalama

Ushirikiano huu mpya, ambao maelezo yake hayajatangazwa, ni "ahadi ya miongo kadhaa", amesisitiza Boris Johnson.

Boris Johnson na Narendra Modi wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko New Delhi, Aprili 22, 2022.
Boris Johnson na Narendra Modi wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko New Delhi, Aprili 22, 2022. AFP - STEFAN ROUSSEAU
Matangazo ya kibiashara

Utiaji saini wa mkataba huu ulifanyika wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Uingereza nchini India. "Vitisho vya kushurutishwa kwa kiimla vimeongezeka zaidi," amesema Bw Johnson akiambatana na mwenzake wa India Narendra Modi, "kwa hivyo ni muhimu tuimarishe ushirikiano wetu."

Ushirikiano huu "mpya na uliopanuliwa" unahusu ulinzi na usalama, kulingana na maneno ya Boris Johnson, ambaye amebaini kuwa nchi hizo mbili zina "maslahi ya pamoja katika kuweka eneo la Indo-Pacific wazi na huru".

Ikiwa maelezo ya ushirikiano huu hayajaainishwa, lengo lake ni "kukabiliana na vitisho vya njia za ardhini, baharini, angan, hasa kwa kuunganisha nguvu kwenye teknolojia ya ndege mpya za kivita na teknolojia ya baharini kugundua na kujibu vitisho. katika bahari,” alisema Waziri Mkuu wa Uingereza.

Majadiliano ya makubaliano ya biashara

Makubaliano hayo yanaendana na matakwa ya New Delhi, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitaka kuimarisha uwezo wake wa kitaifa wa uzalishaji kijeshi, ili kupunguza utegemezi wake kwa nchi za kigeni, haswa Moscow.

Mkataba wa kibiashara pia uko njiani lakini mazungumzo bado yanaendelea. Hasa, serikali ya India inataka visa zaidi kutolewa kwa Wahindi kufanya kazi au kusoma nchini Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.