Pata taarifa kuu

Mabasi yatumwa kuwaondoa raia waliokwama Mariupol

Ukraine imetuma mabasi kwenda kuwapelekea misaada ya kibinadamu watu waliokwama katika mji wa Pwani wa Mariupol lakini pia kuwaondoa kwenye mji huo ambao umekuwa ukishuhudia mashambulizi kutoka kwa wanajeshi wa Urusi. 

Mashambulizi yalisababisha uharibifu wa majengo ya ghorofa wakati wa mapigano nje kidogo ya Mariupol, Ukraine, katika eneo linalodhibitiwa na serikali iliyojitenga ya Jamhuri ya Watu wa Donetsk, Jumanne, Machi 29, 2022.
Mashambulizi yalisababisha uharibifu wa majengo ya ghorofa wakati wa mapigano nje kidogo ya Mariupol, Ukraine, katika eneo linalodhibitiwa na serikali iliyojitenga ya Jamhuri ya Watu wa Donetsk, Jumanne, Machi 29, 2022. AP - Alexei Alexandrov
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya Urusi kutanagza kuwa, inasitisha vita vya isku moja katika mji huo wa Pwani ambao ripoti zinasema watu zaidia ya Laki Moja na Elfu Sabini wamekwama kufuatia mashambulizi ambayo yamekuwa yakiendelea. 

Wakati hayo yakijiri, ripoti za Kiinteljensia kutoka Marekani na Uingereza zinasema Urusi ilidharau uwezo wa Ukraine na watu wa karibui w arais Vmadimir Putin wamekuwa hawamwambii ukweli kuhusu hali inavyoendelea kwenye uwanja wa mapambano. 

Katika hatua nyingine, rais wa Urusi Vladimir Putin ametishia kusitisha usambazaji wa gesi katika nchi ambazo amesema sio rafiki, iwapo hawatotumia sarafu ya nchi yake. 

Hata hivyo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema mataifa ya Ulaya hatokubali agizo hilo la Putin na badala yake, yataendelea kulipia bidhaa hiyo kwa Euro au Dola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.