Pata taarifa kuu

Moscow yadai kwa hakuna 'ahadi' katika mazungumzo na Ukraine

Katika siku ya 35 ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, Jumatano hii, Machi 30, Moscow imefanya mabadiliko na kutangaza kwamba haikuona chochote "cha kuahidi" katika mazungumzo na Ukraine siku ya Jumanne huko Istanbul. Mashambulio ya mabomu yanaendelea.

Picha hii ya setilaiti iliyotolewa na Maxar Technologies inaonyesha nyumba na majengo yaliyoharibiwa huko Mariupol, Ukraine, Jumanne, Machi 29, 2022.
Picha hii ya setilaiti iliyotolewa na Maxar Technologies inaonyesha nyumba na majengo yaliyoharibiwa huko Mariupol, Ukraine, Jumanne, Machi 29, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

►Duru mpya ya mazungumzo ilifanyika Jumanne huko Istanbul. Moscow imesema Jumatano kwamba haikuona chochote "cha kuahidi" katika mazungumzo hayo, baada ya kuyaita "muhimu" siku moja kabla na kuahidi "kwa kiasi kikubwa" kupunguza shughuli zake za kijeshi katika mikoa ya Kyiv na Chernihiv,

►Kwa upande wake, Ukraine inasalia kuwa na mashaka na inaomba makubaliano ya kimataifa ya kuhakikisha usalama wake, wakati jiji la Cherniguiv likikumbwa na mashambulizi ya anga usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano na hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya.

►Mzunguko unaofuata wa mazungumzo hautaendelea leo Jumatano. Nchi za Magharibi zinasema lazima kusiwe na kulegeza msimamo wao dhidi ya Urusi.

►Vikosi vya Ukraine vimezuia mashambulizi ya Urusi kuelekea Brovary, mashariki mwa Kyiv, katika muda wa saa 24 zilizopita. Pia vinadai kuuteka mji wa Irpin, katika vitongoji vya Kyiv, siku ya Jumatatu.

► Takriban watu 5,000 waliuawa huko Mariupol, jiji lililozingirwa na Urusi kwa wiki kadhaa, kulingana na afisa wa Ukraine. Jengo la Msalaba Mwekundu limekumbwa na mashambulizi ya anga leo Jumatano. Umoja wa Mataifa unatafuta kuanzisha maelewano ya "kusitisha mapigano". Jengo la shirika la Msalaba Mwekundu lilikumbwa na mashambulizi ya anga siku ya Jumanne huko Mykolaiv, takriban watu tisa waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.