Pata taarifa kuu

Urusi yaahidi kupunguza operesheni za kijeshi Kyiv

Urusi imetangaza kupunguza mashambulio ya kijeshi katika viunga vya jiji kuu la Ukraine, Kyiv na Kaskazini mwa mji wa Chernihiv, wakati huu mazungumzo kati ya pande mbili yakianza nchini Uturuki.

Binh sỹ Ukraina chuẩn bị lựu pháo ở Zaporizhzhia, Ukraina, 28/03/2022.
Binh sỹ Ukraina chuẩn bị lựu pháo ở Zaporizhzhia, Ukraina, 28/03/2022. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imetangazwa na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Alexander Fomin ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Urusi waliokutana jijini Instabul kwa ajili ya mazungumzo ya ana kwa ana na wenzao wa Ukraine. 

Hili lilikuja baada ya Ukraine katika mazungumzo hayo kutoa mapendekezo ya namna inavyotaka vita vinavyoendelea kukomeshwa. 

Katika mazungumzo hayo ambayo Uturuki imesema ni hatua kubwa ya kumaliza vita nchini Ukraine, ambayo imetaka mataifa ya Magharibi kuihakikishia usalama wake, kwa kuunda kikosi kama au zaidi ya Jeshi la Jumuiya ya nchi za Magharibi NATO. 

Aidha, Ukraine inasema hakikisho hilo, itaachana na mpango wake wa kuwa mwanachama wa NATO, hatua ambayo ni mojawapo ya sababu ya kuvaliwa na Urusi kwa hofu kuwa ikiwa mwanachama, itatishia usalama wake. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.