Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Kiev akataa maeneo salama yanayopendekezwa na Urusi

Katika siku ya kumi na mbili ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Jumatatu (Machi 7), Moscow imeazimia Jumatatu kusitisha mapigano, ili kuwezesha kuanzishwa kwa maeneo salama kuruhusu zoezi la kuhamisha raia kutoka kwa miji iliyoshambuliwa kwa mabomu hadi Belarus na Urusi.

Wakazi wa Irpin, karibu na Kiev, wanajaribu kuhama mnamo Machi 7, 2022.
Wakazi wa Irpin, karibu na Kiev, wanajaribu kuhama mnamo Machi 7, 2022. REUTERS - CARLOS BARRIA
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Ukraine imeona chaguo "lisilokubalika" la njia maeneo salama yanayoelekeza raia kwenda Urusi na Belarus. Jeshi la Urusi siku ya Jumatatu limetangaza kusitisha mapigano ili kuwahamisha raia kutoka miji ya Ukraine ya Kharkhiv, Kyiv, Mariupol na Sumy.

► Duru mpya ya mazungumzo ya Urusi na Ukraine itafanyika Jumatatu hii saa nane usiku saa za kimataifa.

► Jaribio la pili la kuwahamisha raia kutoka Mariupol halikufaulu siku ya Jumapili baada ya jaribio la kwanza kushindwa siku moja kabla kwa sababu ya kutoheshimu usitishaji mapigano. Kutekwa kwa mji huu wa wenye wakazi 450,000, uliyoko kwenye Bahari ya Azov,kungewezesha makutano kati ya vikosi vya Urusi vinavyokuja kutoka Crimea iliyounganishwa, ambayo tayari imechukua bandari muhimu za Berdiansk na Kherson, na vikosi vilivyotangaza kujitenga na vikosi vya rusi katika jimbo la Donbass.

► Katika mahojiano ya simu ya saa 1:45 na Emmanuel Macron, Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema "atafikia malengo yake" nchini Ukraine, "ama kwa mazungumzo au kwa njia ya vita". Amekanusha kuwa jeshi la Urusi "linalenga raia" na akahakikisha kuwa "haikuwa kwa nia yake" kushambulia vinu vya nyuklia vya Ukraine.

► Wakati jeshi la Urusi linakaribia Kiev, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Jumapili kwamba vikosi vya Urusi vinajiandaa kushambulia mji wa Odessa, ulioko kusini mwa nchi hiyo.

Licha ya kukosolewa, Boris Johnson atetea sera yake ya mapokezi

Waziri Mkuu wa Uingereza ametetea sera ya uhamiaji ya serikali yake, akisifu "ukarimu" wake wakati abaini ukaguzi uliosababisha wakimbizi wa Ukraine kukataliwa kuingia bila viza. Kwa sasa, ni visa hamsini pekee ambazo zimetolewa, kwa mujibu wa mwandishi wetu wa London, Émeline Vin.

Emmanuel Macron ashutumu "ukosefu wa kimaadili na kisiasa" wa Vladimir Putin

Rais wa Ufaransa ameshutumu "ukosefu wa kimaadili na kisiasa" wa rais wa Urusi ambaye ametoa maeneo ya usalama kwa wakazi wa miji kadhaa nchini Ukraine "kuwaleta Urusi". Kinachohitajika, ametangaza Emmanuel Macron kwenye kituo cha LCI, "sio tu maeneo salama, hatua ambayo inatishiwa mara moja, sio hotuba ya kinafiki inayosema: "Tutakwenda kuwalinda raia wa kuwaleta Urusi”.

Urusi inaomba ulinzi wa uwakilishi wake nchini Ufaransa

Moscow imedai ulinzi "wa kutosha" wa uwakilishi wake wa kidiplomasia nchini Ufaransa, baada ya "mashambulizi" mabomu ya kienyeji dhidi ya moja ya vituo vyake vya kitamaduni huko Paris. Nyumba ya Sayansi na Utamaduni ya Urusi, iliyoko katikati mwa mji mkuu wa Ufaransa, ililengwa usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, amesema msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi, Maria Zakharova.

Taarifa kuhusu mapambano

Jeshi la Urusi linaendelea kuizingira hatua kwa hatua Kiev, huku mapigano makali yakiripotiwa kaskazini mwa mji huo, karibu na maeneo ya Zhytomyr na Cherniguiv, kilomita 150 kutoka mji mkuu wa Ukraine. Mashambulizi ya mara kwa mara yalilenga pia Irpine, upande wa magharibi, na nguzo zenye silaha zikisonga mbele upande wa mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.