Pata taarifa kuu

Ujerumani yapinga vikwazo vya gesi, mafuta na makaa ya mawe kutoka Urusi

Athari ya kiuchumi ya mzozo uliochochewa na Urusi nchini Ukraine tayari zimeanza kujitokeza. Mnamo Machi 7, mlipuko mpya wa homa kwenye masoko ya kimataifa, baada ya kuongezeka kwa bei ya mafuta na dhahabu na kushuka kwa soko la hisa wakati wa ufunguzi huko Asia.

Novatek, kituo cha kwanza cha kutengeneza treni ya gesi asilia duniani katika kijiji cha Belokamenka, eneo la Murmansk, Urusi, Novemba 29, 2021.
Novatek, kituo cha kwanza cha kutengeneza treni ya gesi asilia duniani katika kijiji cha Belokamenka, eneo la Murmansk, Urusi, Novemba 29, 2021. AFP - NATALIA KOLESNIKOVA
Matangazo ya kibiashara

Swali la kuzuiliwa kwa gesi ya Urusi, mafuta na makaa ya mawe limezua sintofahamu barani Ulaya. Swali lilifutiliwa mbali na Mawaziri wa Fedha na Mambo ya Nje wa Ujerumani.

Ingawa washirika wao wa Magharibi wanajadili kwa umakini sana uwezekano wa kuwekewa vikwazo, Jumapili Machi 6, Mawaziri wa Fedha na Mambo ya Nje wa Ujerumani walisema wanapinga kupiga marufuku uagizaji wa hidrokaboni kutoka Urusi.

Huko Berlin, hawaamini uwezo wa silaha hii dhidi ya Urusi. "Tuko tayari kukabiliana na bei ya juu sana ya kiuchumi. Lakini ikiwa kesho, nchini Ujerumani, taa zitazimaa, hiyo haitazuia mizinga kufanya kazi”. Hivi ndivyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, alijibu, wakati mwenzake wa Fedha alikumbusha hitaji la kushikilia muda dhidi ya Urusi, ambaye ni mvamizi wa Ukraine.

Gesi ya Urusi ni tegemezi

Kusimamisha uagizaji wa gesi, mafuta na makaa ya mawe kutoka Urusi kwa upande mmoja kutatishia amani ya kijamii nchini Ujerumani, kulingana na Waziri wa Ikolojia wa Ujerumani. Kama ukumbusho, Ujerumani inaagiza kutoka Urusi zaidi ya nusu ya gesi yake na 42% ya mafuta yake na makaa ya mawe.

Na itachukua miaka mingi kutoka kwa uraibu huu. Katika azma yake ya kubadilisha vifaa vyake, Berlin ilihitimisha, Jumamosi Machi 5, makubaliano ya ujenzi wa kituo cha LNG kilichokusudiwa kushughulikia gesi asilia iliyoyeyuka. Miundombinu yake ya kwanza ya aina yake.

Homa katika masoko

Kufuatia soko la hisa la Asia, masoko ya fedha ya Ulaya yote yalifunguliwa kwa kushuka sana tarehe 7 Machi. Chini ya 5% kwa CAC 40 na chini ya 4% huko Frankfurt. Na bei za bidhaa zinapanda sana. Bei ya Mafuta ni wazi imepanda kwa kiwango kikubwa. Bei ya pipa la Brent kutoka Bahari ya Kaskazini ilikaribia dola 140 Jumapili jioni. Rekodi kamili tangu mwaka 2008. Moscow ni muuzaji wa pili mkubwa wa mafuta duniani.

Bei ya gesi pia inaongezeka. Bei yake ya Ulaya ilipanda kwa 60%, hadi zaidi ya euro 300 ya megawati kwa saa. Baadaye, bei ya malighafi imepanda. Metali ni sekta muhimu, inayosafirisha kutoka Urusi hadi Ulaya. Mzozo na Ukraine pia umesababisha kuongezeka kwa bei ya alumini, shaba na nikeli. Na dhahabu, inayochukuliwa kuwa kimbilio salama, inaendelea kuongezeka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.