Pata taarifa kuu

Ufaransa: Pasi ya chanjo yaidhinishwa na Bunge

Bunge la Ufaransa limepitisha Jumapili hii Januari 16, kwa kura ya mwisho ya wabunge, muswada wa kupitishwa kwa pasi ya chanjo, ambayo serikali inataka kutekeleza haraka iwezekanavyo katika kukabiliana na kuzuka tena kwa janga la Covid-19.

Manifestation contre le passe vaccinal, à Paris le samedi 8 janvier 2022.
Manifestation contre le passe vaccinal, à Paris le samedi 8 janvier 2022. © AP - Adrienne Surprenant/
Matangazo ya kibiashara

Nakala hiyo imepitishwa kwa kura 215 dhidi ya 58, huku wabunge 7 wakijizuia kupiga kura. Wabunge wa kisoshalisti wamepanga kufikisha malalamiko yao katika Baraza la Katiba ili kuhakikisha "uhuru wa kimsingi" umeheshimiwa, hali ambayo itaahirisha kutangazwa kwa muswada huo kwa siku chache.

Hivi karibuni Ufaransa ilitangaza vikwazo vikali vya Covid, huku kukiwa na wasiwasi juu ya kirusi kipya cha Covid, Omicron.

Pasi ya chanjo iliyopangwa ya Ufaransa - ambayo itahitaji uthibitisho wa chanjo, sio tu kipimo hasi, ili kuingia kwenye maeneo ya umma - ingelianza kutekelezwa kuanzia Januari 15,  ikiwa bunge lingeidhinisha muswada wa sheria hiyo kabla ya tarehe hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.