Pata taarifa kuu

Ufaransa: Wabunge wapitisha mswada wa sheria ulioibua mjadala kuhusu chanjo

Nchini Ufaransa baada ya mjadala wa siku tatu bungeni, wabunge wamepitisha mswada wa sheria, unaowataka watu wote nchini humo kuonesha cheti cha kupata chanjo ili kuruhusiwa kuingia kwenye maeneo ya umma kama migahawa na majumba ya Cinema.

Waziri Mkuu Jean Castex anazungumza mbele ya wabunge, Jumatano hii, Januari 5, 2022.
Waziri Mkuu Jean Castex anazungumza mbele ya wabunge, Jumatano hii, Januari 5, 2022. AFP - BERTRAND GUAY
Matangazo ya kibiashara

Wabunge 214 wamepitisha mswada huo huku 93 wakipinGa na sasa utajadiliwa na Maseneta wiki ijayo. Serikali ya Ufaransa ilikuwa imepanga sheria hiyo ianze kutumiwa kuanzia Januari 15.

Hayo ni baada ya Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex kuepo bungeni Jumatano hii, Januari 5, baada ya mkutano uliogubikwa na maswali mengi siku moja kabla, kufuatia matamshi ya kutatanisha ya rais wa Jamhuri juu ya "nia" yake "kukabaliana" na wale ambao hawakuchanjwa.

Waziri Mkuu wa Ufaransa alitoa wito kwa wabunge "kujadiliana haraka iwezekanavyo" kuhusumuswada wa kuanzishwa kwa hati ya chanjo, uchunguzi ambao ulikuwa umesitishwa Jumanne jioni katika hali tete.

"Ni jukumu lenu kujadili haraka, kwa kuzingatia hali ya nchi yetu, ya Ulaya", amesema Bw. Castex Jumatano hii mbele ya Bunge, siku moja baada ya kikao chenye kilichokubikwa na maswali mengi.

Waziri Mkuu alirejelea kauli ya Emmanuel Macron kuhusu wale ambao hawajachanjwa kwa masharti haya: “Kuna ugumu wa wananchi wenzetu wanaokataa kuchanjwa. Hapa sijamtukana mtu, ni ukweli. "

"Kuwa huru haimaanishi kuwaambukiza wengine bila kuadhibiwa, si kusumbua idara zetu za afya ambazo tayari zinakabiliwa na mambo mengi," amebaini Jean Castex, akitaka "jukumu la kibinafsi la kila raia wa Jamhuri."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.