Pata taarifa kuu
UFARANSA

Ufaransa: Emmanuel Macron azindua mkutano wa uhifadhi wa uasilia duniani

Kongamano la kimataifa la Umoja wa Kimataifa wa Kulinda Uasilia (UICN) limeanza tangu Ijumaa wiki hii huko Marseille, kusini mwa Ufaransa, chini ya uenyekiti wa Emmanuel Macron.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Marseille, Septemba 3, 2021.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Marseille, Septemba 3, 2021. © REUTERS/ Guillaume Horcajuelo/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kwa kufungua mkutano huo, rais wa Ufaransa ameahidi kwamba Ufaransa itakuwa tayari kulinda vema nafasi yake ya baharini katika Mediterania ifikapo mwaka 2027.

Mkutano wa IUCN,  International Union for the Conservation of Nature, umeanza kama ilivyo kuwa imepangwa, ameripoti mwandishi wetu maalum huko Marseille, Agnès Rougier.

IUCN ni Jumuiya ya Kimataifa ya Kulinda Uasilia, ambayo inajumuisha vyama na mashirika yasiyo ya kiserikali, na pia mashirika ya umma, wawakilishi wa mataifa kama jamii kutoka nchi mbalimbali duniani.

Uasilia, maana yake ni ulimwengu ulivyo kwa asili, kabla ya binadamu kuuathiri kwa utamaduni na hasa kwa ustaarabu wake, uliokuza teknolojia inayomwezesha kufanya mengi, mazuri na mabaya, pengine mambo yanayoleta faida ya haraka lakini yana madhara makubwa kwa siku za mbele.

Katika miezi iliyotangulia mkutano huo, wanachama wa IUCN walipendekeza hoja zinazoshughulikia sekta zote za ulinzi wa bioanuwai: ukataji miti, vita dhidi ya usafirishaji wa spishi, kilimo endelevu au ulinzi wa bahari. Na hoja hizi zitajadiliwa kuanzia Jumamosi hii na kwa kipindi cha wiki moja, katika vikao mbalimbali, mikutano na warsha. Wanasayansi wengi wanashiriki katika mkutano huo, na pia ni fursa kwao kukutana na wanachama wa mashirika ya kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.