Pata taarifa kuu
DRC-UVIRA-MVUA-MAZINGIRA

Mafuriko: Hofu yatanda kwa wakazi wa Uvira

Wakazi wa Uvira, katika Mkoa wa Kivu Kisuni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanahofu ya kutokea mafuriko me makubwa na kusababisha vifo zaidi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Uvira en RD Congo, depuis un hélicoptère Puma de la MONUSCO.
Uvira en RD Congo, depuis un hélicoptère Puma de la MONUSCO. Photo MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Mvua kubwa iliyonyesha katikati mwa wiki hii ilisababisha mafuriko yaliyowaua makumi ya watu mjini wa Uvira.

Mvua inayonyesha ikiandamana na upepo mkali imesababisha mito kufurika na kuleta maafa sio tu katika mji wa Uvira lakini pia sehemu zingine za DRC.

Kwa sasa raia wengi hawana makazi wengi nyumba zao zimesombwa na maji ya mafuriko hayoyaliyosababishwa na mvua.

Kwa mujibu mamlaka katika eneo hilo, idadi ya vifo imepanda kutoka watu 15 hadi zaidi ya 25 siku ya Jumamosi, na huenda idadi hiyo ikaongezeka kwa mujibu wa mashahidi.

Zoezi la kuwatafuta manusura linaendelea, kwa mujibu wa mashahidi mjini Uvira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.