Pata taarifa kuu
WAHAMIAJI

Idadi ya wahamiaji waliokufa maji baharini yaognezeka mwaka 2021

Katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu wa 2021, watu wasiopungua 1,146 walikufa maji baharini wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterranean kuingia Ulaya, kulingana na Shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM)

Maafisa wa uokoaji wakisafirisha mwili wa mhamiaji aliyekufa kwenda pwani ya Orzola katika Kisiwa cha Canary cha Lanzarote, Uhispania, Juni 18, 2021.
Maafisa wa uokoaji wakisafirisha mwili wa mhamiaji aliyekufa kwenda pwani ya Orzola katika Kisiwa cha Canary cha Lanzarote, Uhispania, Juni 18, 2021. REUTERS - BORJA SUAREZ
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya wahamiaji waliokufa maji baharini wakijaribu kuingia Ulaya imeongezeka zaidi ya mara mbili mwaka huu, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema Jumatano wiki hii, huku likitoa wito kwa mataifa kuchukua hatua za haraka.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na IOM katika ripoti mpya, watu wasiopungua 1,146 walikufa maji baharini wakijaribu kuingia Ulaya katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2021.

Mnamo mwaka wa 2020, watu 513 walikufa maji kwa kpindi kama hicho, na watu 674 walikufa maji mwaka 2019.

"Mashirika yanayotoa msaada kwa shughuli za uokoaji wa raia yameendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali, na boti zao nyingi zimekwama katika bandari za Ulaya kutokana na kesi za jinai dhidi ya wafanyakazi wa boti hizo.", Inabainisha ripoti hiyo. IOM pia inabainisha kuwa ongezeko la vifo linakuja wakati ambapo vizuizi vya boti zinazobeba wahamiaji kutoka pwani ya Afrika Kaskazini vinaongezeka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.